Nanyaro aokoa wanafunzi kutembea kilomita 3 kuchota maji

MDAU wa maendeleo mkoani Songwe, Ombeni Nanyaro amechangia kiasi cha Sh. milioni moja kwa ajili ya kuunganisha maji na kukarabati bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari Kamsamba wilayani Momba mkoani Songwe. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe… (endelea).

Nanyaro ametoa kiasi hicho cha fedha baada ya kutembelea shule hiyo inayomilikiwa na jumuiya ya wazazi (CCM) na kushuhudia wanafunzi wakitembea umbali wa kilometa tatu hadi mtoni kusaka maji ambayo si safi na salama.

Akizungumza na MwanaHALISI jana Nanyaro mbaye pia ni mjumbe wa bodi ya shule hiyo na mjumbe wa mkutano Mkuu CCM mkoa, amesema tayari ameunganisha maji safi na wanafunzi wameanza kuyatumia.

Pia amesema mpango uliopo ni kununua vitanda na magodoro ikiwemo kulikarabati bweni la wanafunzi kwani limechakaa.

“Naahidi nitayakamilisha haya niliyoanza kuyafanyia kazi lakini pia nitaweka computer  katika madarasa ni na tv kwenye mabweni ili wanafunzi wajisikie wapo nyumbani,” amesema.

Suma Mwashitete mmoja wa wanafunzi shuleni hapo, pamoja na kushukuru kwa msaada huo, amesema wataepukana na vihatarishi mbalimbali pindi walipokuwa waenda kuchota maji.

Akizungumza kwa niaba ya wazazi wenzake shuleni hapo Sarafina Nakandonga amesema mjumbe Nanyaro ana moyo wa kipekee na wameshuhudia ameyafanya mengi ndani ya mkoa wa Songwe.

Related Posts