Picha :Mwili wa mtoto asimwe aliyeuawa kikatili Muleba,azikwa nyumbani kwao

Ni picha kutoka nyumbani ulipopumzishwa mwili wa mtoto Asimwe mwenye zaidi ya miaka miwili aliyekuwa albino

Mtoto huyo aliibwa nyumbani kwao Mbale kijiji Bulamula kata ya Kamachumu Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera May 30 2024 na mwili wake umekutwa umetelekezwa kwenye karavati eneo la kata Ruhanga Tarafa Kamachumu Wilayani Muleba siku ya jana June 17 huku baadhi ya viungo vikiwa vimekatwa

Mazishi hayo yamesimamiwa na Serikali yakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera

 

Related Posts