Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KUNA mambo lazima tuzungumze japo kwa lugha yoyote ambayo unaweza kuitumia lakini ikasaidia kufikisha ujumbe kwa uliowakusudia na hasa Watanzania wenzangu.
Leo kuna jambo nataka kulisema,kulizungumza,kuna jambo nataka kulisimulia.Nikuombe kama uko tayari usome kuanzia mwanzo mpaka mwisho, kama unadhani hutaweza ni bora usisome. Kwanza sijakuandikia wewe.Iloooo.
Sasa ndugu yangu, rafiki na jamaa yangu na kubwa zaidi Mtanzania mwenzangu ujue nimekaa na kutafakari sana kuhusu uongozi wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan, nimewaza jinsi anavyoongoza nchi, jinsi anavyotoa maelekezo, jinsi anavyotekeleza miradi ya maendeleo.
Katika kuwaza na kuwazua, kutafakariii weeeee,nikajikuta nasema Mungu Muumba mbingu na ardhi ahsante kwa zawadi ya Mama huyu, Mama wa Taifa la Tanzania,raia namba moja,kiongozi mahiri na hodari Dk. Samia Suluhu Hassan.
Tunajivuna kuwa na Rais Samia Suluhu Hassan,udongo wa ardhi ya Tanzania pale Kizimkazi Unguja visiwa vya Zanzibar vyenye harufu ya marashi ya karafuu.Tunakushukuru Mwenyezi Mungu kwa kufanya Mama yetu Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wetu.
Hakika chini ya uongozi wake nchi imetulia,nchi inasonga, nchi inapiga hatua. Wenye macho tunaona, wenye masikio tunasikia.
Najua wapo baadhi ya watu wanajiuliza huyu jamaa imekuaje mbona anamfagilia sana Rais? Ukweli kwa mwenye akili timamu na haya anayofanya Rais Samia lazima utampongeza.
Tufanye hujui kusoma basi hata picha huoni? Acha mambo yako.Kumsifia anayefanya vizuri wala sio dhambi, acha nimsifu na kumpongeza Rais Samia. Mama hongera kazi unayofanya Watanzania tunaiona, piga kazi,songa mbele.
Na juzi wakati anasimulia ile hadithi ya Chura kiziwi aliyepanda juu ya mti; Rais alisema kulikuwa na mashindano ya chura kupanda juu ya mti lakini wakati wanapanda kelele za kwamba hatawaweza zilikuwa nyingi.
Kelele za kwamba hawatafika zikawa nyingiii ,Chura wengi walishuka lakini mmoja alipanda hadi juu ya mti na kisha akashuka , wenzake wakawa wanashanagaa amewezaje.
Aliposhuka wakaanza kuuliza amewezaje? Kumbe Chura yule alikuwa kiziwi,hasikii kilichokuwa kinasemwa, hakusikia kelele.Sasa pata hicho kisa hicho kwa sauti ya Rais Samia jumlisha na lile pozi lake ,utapendaaa.Ila hapo kwenye pozi lake fanya kama hujaona,kama hujasoma.
Hakika hadithi ya Rais Samia kuhusu CHURA KIZIWI ukiitafakari kwa kutulia utaibaini sababu za kufanikiwa kwake,sababu za nchi yetu kutulia ukisikiliza simulizi hiyo utabaini kwanini Rais Samia amefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati iliyogharimu mabilioni ya fedha.
Ukitaka kujua ukweli wa hilo aangalia Mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, Watanzania tumeanza kuonja utamu wa mradi huo, mgao wa umeme hakuna,sio ule tena wa asubuhi upo, mchana hakuna, jioni hakuna usiku upo.Ni mwendo wa majenereta.
Kuanza kufanya kazi kwa baadhi ya mitambo ya mradi wa umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere tunashuhudia kutokuwa na mgao.Basi kama nikisema hakuna mgao unaona naongopa, basi sema tu hivi sasa hali si kama ilivyo zamani
Tumefika hapo kwasababu Rais Samia amebeba maono makubwa na lengo lake ni kuhakikisha Watanzania tunakuwa na umeme wa uhakika. Halafu Rais anavyojua kuchanga karata zake akamchukua Dk.Dotto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu halafu ndio Waziri wa Nishati.
Kwa mazingira hayo mradi unakwamaje? Rais ana maono na Dk.Biteko anajua kutekeleza maono ya Rais. Leo mtambo namba nane tayari umewashwa na umeme umeingia kwenye gridi ya Taifa.
Hapa niko zangu Majohe Kwasonga naangalia Golden Boi, umeme upo, halafu sina pakwenda.Acha nimuangilie Ferit na mkewe Seirani, dogo noma sana huyu, ni wale watu tunaosema Samu taimu no,samtaimu yesi.
Lakini Rais Samia sio tu kwenye kutekeleza mradi wa umeme wa Mwalimu Nyerere, nenda kwenye mradi wa daraja la Kigongo-Busisi kule Kanda ya Ziwa, kasi ya utekelezaji mradi ni kubwa.
Walioko Mwanza na Kanda ya Ziwa wanajua kinachoendelea. Halafu nakaaje kimya,Rais anastahili pongezi .
Achana na mradi wa daraja la Kigongo-Busisi,njoo kwenye ujenzi wa reli ya kisasa inayotumia umeme,tumezoea kuiita reli ya treni ya mwendo kasi maarufu SGR.Leo hii tayari safari za treni Dar – Moro zimeanza. Halafu mama Samia alivyokuwa na hatari nauli elfu 13 kwa mtu mzima na mtoto elfu sita.
Nikisema 2025 kura zote kwa Samia nitaonekana namfanyia kampeni, lakini kwa kasi hii ya maendeleo tunaachaje kumpigia debe.Kura yangu hakika ni mali yake, ya kwako kama unaona kero subiri atakayesimamishwa na vyama vya upinzani na bahati mbaya hata simuoni.Achana na hayo.
Njoo katika elimu Rais Samia si tu ameongeza fedha katika ujenzi wa miundombinu ya sekta ya elimu,amekwenda mbali zaidi hata fedha za mikopo kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu nazo kaongeza .
Rais Samia anajua bwana .Siku hizi zile habari za watoto wanaokwenda kidato cha kwanza wasuburi madarasa yajengwe hakuna tena .Unacheza na Samia wewe.Acha Kabisa.
Anafanya yote hayo halafu yuko kimyaaa, wala hana makuuu,wala haringi. Ukifuatilia aina ya uongozi wake utabaini anaongoza kama Rais lakini ametulia kama Mama. Hana kelele na familia inakwenda.
Ingekuwa wanaume hapo hata panya angejua kama daraja la Wami sasa madereva spidi 120 halafu abiria Wala hatujui Kama tuko Wami.Zamani kupita Wami ilikuwa roho juu.Wale ndugu zangu wa Mikoa ya Kaskazini wanapajua vizuri Wami.Leo imebakia historia.Hongera kwa Rais Samia.
Hata katika Kilimo Rais Samia amefanya mageuzi makubwa, wakulima wanaonja ladha halisi ya uongozi wa Mwanamke Shupavu,Mwanamke wa Shoka,Malkia wa Nguvu Rais Dk Samia Suluhu Hassan. Zile kelele za mbolea kuchelewa hakuna tena .
Mama kaweka mipango kisha kampa kijana mdogo kutoka pale Nzega Mjini Hussein Bashe kuwa Waziri wa Kilimo ili kusimamia utekelezaji wake.
Tunashuhudia wakulima ambavyo wananufaika na kilimo chao,miradi ya miundombinu ya umwagilaji mama amepeleka mabilioni ya fedha.Muulize Bashe atakueleza vizuri.
Katika sekta ya maji huko ndio balaa, Rais ameamua kumtua ndoo mwanamke kichwani,nenda vijiji utajua nazungumzia nini.Kuna maeneo tangu kuumbwa kwa Dunia hawahi kupata maji safi na salama,ilikuwa wao na mtoni,wao na kwenye mabwawa .
Lakini chini ya Rais Samia maji safi hadi vijijini.RUWASA wanaifanya kazi ya Rais Samia kwa umakini mkubwa. Na kazi ya kupeleka maji vijijini inaendelea .
Waziri wa Maji ni Jumaa Aweso halafu kazi anaipenda na Uwaziri wa Maji anautaka.Yeye na Watendaji wake muda wote wanawaza jinsi gani watatimiza lengo la Rais la kumtua mwanamke ndio kichwani.
Ngoja tufanye hivi kwa ufupi tu, Rais Samia anastahili pongezi,anastahili kila aina ya sifa. Kazi anayofanya sote tunaona.Dar es Salaam leo ujenzi wa miundombinu ya barabara za mwendo kasi iko kila kona .Hata sisi wa Gongolamboto tumeanza kuona nyota njema.
Ujenzi unaendelea kwa kasi. Kama namuona Mkuu wa Mkoa wangu wa Dar Albert Chalamila.Anafuatilia ujenzi kwa jicho la uwindaji.Nani asiyependa mambo Mazuri.
Kwa spidi ya Rais Samia katika ujenzi wa miundombinu hata wakazi wa Majohe kwanzoma tuna matumaini,Tukijengewa barabara yetu ya Majohe kupita Halisi hadi kwa Mpemba atakuwa amepiga bao.
Rais Samia kwa utekelezaji huu wa miradi ya maendeleo hakika watanzania tunakupenda sana,tuko pamoja na wewe.Tunakuombea afya na uzima .
Tunaisubiria kwa hamu 2025 tukajipange kwenye foleni kuhakikisha unarudi katika nafasi ya urais ili tuendelee kujenga nchi yetu .Kura yangu na hata za Watanzania wengine zaidi ya milioni 60 zinakusibiria .Hakuna cha kukulipa zaidi ya kukupa heshima katika boksi la kura.
Kwa lugha rahisi nasema hivi mwaka 2025 kwa Rais Samia mitano tena.Wenye kununa na Wanune.shauri yao, Rais Samia endelea kuwa kiziwi,watumikie Watanzania kwani wanakuamini, wanaona unayoyafanya.
Nakumbuka hata wakati ule unazungumza kuhusu maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam kuna watu walibeza na kukebehi,lakini juzi wameshuhudia mabilioni ya fedha yaliyotolewa na Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) kama gawio kwa Serikali.Rais Samia ahsante kwa Nia yako njema na Taifa hili.
Lakini kabla ya kuhitimisha naomba niseme kwa unyenyekevu mkubwa.Hakika Rais Samia moyo wangu unamwambia nakupenda sana halafu I Love You.
Kwa kazi kubwa na nzuri unayofanya kwa Taifa hili kwa niaba ya Watanzania wengi tunasema tunakupenda, Tutakulinda na tutakuthamini.
Achana na wale wanatoa lugha chafu,lugha za kejeli na lugha za matusi kwa Rais. Wasikusumbue,wasikupe tabu na wengine hata hapa wapo.Wamesoma kuanzia mwanzo mpaka mwisho wanasema hakuna lolote.
Kwanza na mimi kama Chura Kiziwi,sisikii kama ambavyo Rais hasikii yale yanayosemwa na wale wenye akili na mawazo kama yuleeee ….(Simtaji).
Yaani mtu anakunja sura kabisa,oooo jamaa anasifia tu, sawa tufanye nasifia.We ulitakaje? Acha roho mbaya. Acha choyooo haitakusaidia. Lakini nakubali Rais naye ni binadamu sio Malaika, hivyo si mkamilifu. Tunayo nafasi ya kumvumilia.
Kwa ujumla tunaridhika na uongozi wake.Nchi umetulia,nchini inasonga, kila mtu ana amani ya moyo.Anauhakika na kazi anayofanya. Ila narudia tena Rais Samia nakupenda sana halafu I Love You.
Kasimu 0713833822.