RAIS WA IPU DKT.TULIA ATETA NA WAWAKILISHI WA BUNGE LA MAREKANI

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Waheshimiwa Wawakilishi wa Bunge la Congress la Marekani wakiongozwa na Mhe. Vern Buchanan, katika Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam leo tarehe 18 Juni, 2024.

Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wamejadili kuhusu namna ya kuendeleza ushirikiano na mahusiano bora ya kibunge baina ya Tanzania na Marekani kwa maendeleo ya wananchi wa nchi hizo mbili.  

Related Posts