TETESI ZA USAJILI BONGO: Pa Omar Jobe kuikamua Simba Sh200 milioni

Simba imepanga kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wake Pa Omar Jobe kwaajili ya msimu ujao.

Jobe alijiunga na Simba katika dirisha dogo la Januari kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu lakini ufanisi wake haujawaridhisha.

Simba inamtoa Jobe kwa Mkopo ili kusdajili mshambuliaji mwingine kwani kama itamvunjia mkataba itahitajika kumlipa zaidi ya sh200 mil.

Azam ipo kwenye hatua za mwisho kuachana na aliyekuwa beki wake, Msenegal Malickou Ndoye. Ndoye alijiunga na Azam mwaka 2022 akitokea Teungueth ya kwao Senegal na kuanza maisha ndani ya Azam Complex kwa kiwango bora lakini baadae aliandamwa na majeraha yaliyomfanya muda mwingi kukaa nje ya uwanja.Mkataba wa Ndoye unatamatika mwezi huu.

SIMBA Queens imeanza mazungumzo na viungo wa Yanga Princess, Saiki Atinuke na Precious Christopher ambao mikataba yao iko mbioni na klabu hiyo. Inaelezwa viongozi wa timu hiyo wamechungulia mikataba ya wachezaji hao wa kigeni na ofa walizopewa na klabu yao jambo lililowapa nguvu viongozi wa Simba kuhakikisha wanamwaga noti kuwapata.

JKT Queens imemuongezea mwaka mmoja straika wa timu hiyo, Yasinta Mitoga (17).

Kinda huyo alibakiza mkataba wa miezi sita hivyo kutokana na kiwango alichooonesha mwishoni mwa msimu imeshawishio viongozi wa timu hiyo kumpa mwaka mmoja wa kumtazama.

BAADA ya kumfuatilia kwa wiki sasa hatimaye Simba Queens imekubaliana na beki wa kati wa Wiyeta FC ya Kenya, Lorine Ilavonga ambaye alikuwa pia akiwindwa na Police FC ya Kenya.

Msimamizi wa mchezaji huyo kinda mwenye miaka 17 inaelezwa baada ya kuletewa ofa hizo jicho lilikuwa Tanzania kutokana na uwezekano wa  mshahara na posho.

KIUNGO Zawadi Mauya huenda msimu ujao akaichezea klabu ya Singida Black Stars (Zamani Ihefu), baada ya mkataba wake na Yanga kufika ukingoni.

Tayari viongozi wa Singida na Mauya wamefungua mazungumzo ya kusaini mkataba wa miaka miwili huku Yanga ikionekana kutomuhitaji tena Mauya aliyejiunga na chama hilo 2020 akitokea Kagera Sugar.

MASHUJAA iliyonusurika kushuka daraja, imepeleka ofa kwa Mtibwa Sugar ili kumnasa kipa Mohamed Makaka, kuongeza nguvu kikosini baada kuwepo kwa taarifa kipa Erick Johora amemaliza mkataba ndani ya timu hiyo ya Kigoma. Makaka bado ana mkataba na Mtibwa iliyoshuka daraja. 

Related Posts