https://p.dw.com/p/4hCn3
Makundi ya Kiraia yamesema maandamano hayo na mpango wa kukaa mbele ya jengo la bunge vitaendelea licha ya waandamanaji wenzao 210 kukamatwa.
Kamanda wa Polisi wa Nairobi Admason Bungei amesema hakuna kundi lililoruhusiwa kuandamana mjini humo.
Mapema, polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya mamia ya waandamanaji na kusababisha biashara kufungwa kwa muda kutokana na hofu ya uporaji.