Kim Jong Un aahidi kuiunga mkono Urusi kwenye operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine

Mitaa ya mji mkuu wa Korea Kaskazini Jumatano ilijaa umati wa watu wenye shangwe, wanajeshi waliofurika mitaa mbali mbali na sio kwa Kim Jong Un, lakini kwa mgeni wake na mshirika anaemtegemea kwa sasa, Vladimir Putin.

Katika ziara hiyo ya nadra katika taifa hilo lililojitenga lenye silaha za nyuklia, kiongozi wa Urusi na mwenyeji wake walitia saini ushirikiano wa kimkakati wa kina ambao unaweza kuimarisha ushirikiano wao wa kijeshi na kiuchumi huku nchi zote mbili zikikabiliwa na vikwazo vingi vya kimataifa na makabiliano na Marekani na washirika wake.

Makubaliano hayo yanaweza kupanua uhamishaji wa teknolojia ya kijeshi kwenda Pyongyang badala ya usambazaji wa silaha ambazo jeshi la Moscow linahitaji sana kwa vita vyake vya Ukraine.

Maafisa wa Marekani hapo awali waliiambia NBC News kwamba uhamisho huo unaweza kuimarisha uwezo wa nyuklia wa Korea Kaskazini na kutishia eneo la Asia-Pasifiki.

Kim, ambaye amekuwa akiharakisha majaribio ya silaha na kuzua mvutano na mshirika wa Marekani Korea Kusini, Jumatano aliahidi “uungaji mkono wake kamili” kwa kile Urusi inachokiita “operesheni yake maalum ya kijeshi” nchini Ukraine.

Putin alitembelea Pyongyang mara ya mwisho mwaka wa 2000 ili kuboresha uhusiano na babake Kim, Kim Jong Il, wakati ziara ya kiongozi wa sasa wa Korea Kaskazini  mashariki ya mbali ya Urusi mwaka jana ilitoa dalili za kuimarika kwa uhusiano huo.

Related Posts