Iko uliza wajiri ya kilimo na juluku na samaha ya kodi kampuni ya fukoni? Kama napigia yeye kelele, nageuka chura. Kama veve napiga kelele kama pinjani, chura nakaa kimya. Kama nazidi kelele. Yeye naonya hapana kanyaga guru vake nauza. Sasa iko ogopa sana. Kama rahis nageuka nyoka hapana umma umma sana? Kama nageuka chatu hapana kula vote na yote dugu yangu?
Sasa mimi anza ogopa sana hii sanii. Bila fanya sanii mambo yako yote naharibika kabisa. Vatu nafanya sanii ili naishi. Nageuka chawa. Nyingine nageuka kunguni. Nyingine nakuwa fyatu nafyatua njuluku ya chovu na sikini. Kila moja iko sanii. Kama hapana jua sanii, napotea na kuteseka vakati vote dugu yangu.
Juzi nakwenda Bombei kuona bibi na toto. Naacha yeye na toto moja nakuta toto tano na yote nakuwa sanii. Nakwenda sule nataka Ipad. Narudi Tanjania nakuta kila kitu sanii kila Swahili hata Hindi sanii. Sirkal nafanya sanii ya kupiga juluku. Naanzisha tozo na chango mpaka tumboni nauma. Kuku nakuwa sanii nataga yai ya rangi. Bila kuwa sanii, maisha iko tabu sana.
Siku nafatuka ile mendazake Kufuli mimi dhani kaya kuwa ya Samier siyo ya sanii. Sasa kila kitu naona sanii. Profesa sasa nayo nageuka sanii ya siasa kabisa. Iko mingi naingia siasa. Vatu nafanya sanii kwelikweli. Nafanya sanii ya nguvu sana dugu yangu. Kama nakopa juluku, nakausa damu. Hii naona penzi ya sanii. Veve kopa ile kopo umiza umiza.
Inji yote jaa sanii na chawa ile kunguni. Napenda sana sanii na sanii napenda sana yeye. Juzi ile dege kubwa kubwa inajaa sanii mingi kwa juluku ya sikini ya kaya. Na vana kaya nafanya chura. Hapana lalamika kwa nini aache vakulima. Toto sanii. Sasa naimba stari ya rap. Hapana soma suleni. Nataka tengeneja juluku kuba harakaharaka kama Kanjibhai. Vatu kuba sasa sanii nasifia sifia Samier kupata njuluku.
Kama nachukia au nakataa sifia yeye, nakufa sikini dugu yagu. Kama veve iko sanii, nasahau Mungu, nasifia vatu nene. Vyuo sanii. Sasa natoa honoris causae kama jugu. Sasa kaya nakuwa ya doktori sanii mingi sana. Sanii nayo nakuwa sanii ya siasa. Nagombea jengoni. Natumia vana siasa fanya sanii kule mtaani.
Hii kaya basi iite saniiland. Hindi nakuwa sanii. Kama naongea swahili, nabukanya. Kama nakamatwa na data, naongea swahili kuliko Zaramo. Chukuaji nayo sanii. Sasa naita wekejaji. Ile miji kubakuba sana hesimiwa. Nafanya sanii. Napata tumboni kuba na kila kitu kubakuba. Nakuwa na nyumbani dogo mingi. Nyingine nabaka toto za chuo. Yote hii sanii ya siasa.
Sanii sasa mali kuliko dukani. Kama nataka juluku kuba, lazima iwe sanii ya siasa. Naendesa dukani na kugombea bungeni na kupiga juluku. Sirkal kila maka nanunua sangingi. Naharibu. Nauza mnada kwa bei ya sanii na sanii kuba napata deals.
Kama veve sikini nafanya kazini na nastaafu, napewa kinua gongo ya sanii. Napewa kidogo. Kikuba naweka sirkal. Natumia kama hapana akili njuri. Chovu nalalamika. Veve nanyamaza kama chura. Sirkal nafanya sanii. Nasema navekea veve juluku yako! Kama nakupa yote nakwenda lewa pombe na kufa haraka. Je, kama nanyima veve juluku yako, hapana tatizo fyatua veve na kufa haraka jamani? Hii yote sanii.
Pinjani napiga kelele sana kama kisimani ya maji. Ile chura kuba naziba sikio. Napiga juluku toto, mama, na rafiki. Vote napiga juluku. Sikini sanii nalala sikini naamka tajir. Sasa na pinjani nayo kama nageuka chura, nani tapiga kelele ile chura kuba na nyingine napiga juluku? Kama yeye chura, basi pinjani chemsa maji naunguza chura. Kama nafanya jusi, pinjani bana lango.
Ile vatu ya dini nayo siku hizi sanii. Naimba nyimbo ya siasa sanii. Nasifia ile chura kuba napata juluku. Nyingine nafanya sanii. Nadanganya jinga nafanya ujiza. Napata juluku. Naendesa gari kuba. Nalala kwa jengo kuba. Ile sikini nafanyia sanii naambia omba Mungu. Nafanya sanii. Naita ujiza. Kanji iko kataa ujiza.
Vajinga ndiyo valivao dugu yangu. Chunga sana sanii ya dini na sanii ya siasa. Siku hiji sanii ya dini na sanii ya siasa nalala tanda moja. Kama nataka kuwa sanii, hapana chukia witu baya. Veve sifia. Kama napigwa kofi cheka. Kama juluku yako napigwa, sema namwaga juluku.
Sanii nyingine, sirkal nakopa juluku. Natumia wibaya. Hapana taka swali howo howo. Nafanya kataba hatari jaa sanii. Hapana taka swali. Nauza fyatu fyatua fyatuliwa. Hapana taka swali. Nafanya kaya kama dukani, chovu na fyatu natazama tu kama chura! Chama sasa nakula kitu yote. Kama nauliza nini bana? Nasema yeye chama twavala. Natavala na kula. Hiyo ndiyo kazi ya chama tavala. Kama napinga veve, iko adui ya kaya nachapa viboko.
Kama nataka kwenda bungeni, lazima sifia. Kama nanyimwa rodi ya jimboni yako, napiga sarakasi jengoni. Kama nabana vaziri swali gumu, chama naita veve. Kama nabisa, nenda uliza ile Vanga Mpini. Kama naleta domo kuba, chura nene nasema veve itengwe. Tena iko ongeza kuwa veve laani. Nakumbuka ile Nipe Pepe nneiye nasema jengoni? Nasema pinjani yote laana.
Du! Kumbe naota niko Bombei na nimegeuka Napharata Karanāra bin Jātivādī bin Cōra! Bhagavāna manē madada karē. Kwaheriiii!