Wilder, Fury waporomoka WBC | Mwanaspoti

BONDIA wa ngumi za uzito duniani (Heavy Weight), Deontay Wilder ameporomoka kwenye viwango vya ubora kwenye mchezo huo, huku Tyson Fury akimpisha Oleksandr Usyk namba moja.

Wilder ambaye anasubiriwa kutoa kauli juu ya hatma yake kwenye mchezo huo baada ya kuchapwa kwa Knockout ‘KO’ mara mbili mfululizo na mambondia Joseph Parker na Zhilei Zhang, ametupwa hadi nafasi ya 15 ambayo hajawahi kushuka kwa kiwango hicho.

Miaka mitano nyuma, bondia huyu Mmarekani alishika nafasi ya kwanza kabla ya vipigo hivyo mfululizo kumwondoa kwenye ubora huo na hatma yake amebaki nayo mwenyewe vya kama ataendelea na masumbwi au ataachana nayo.

Kwenye orodha hiyo, Usyk raia wa Ukraine sasa anaongoza sambamba na Mwingereza Anthony Joshua huku nafasi ya pili akishika Fur.

Usyk alimchapa Fury aliyekuwa bingwa wa Mkanda wa WBC, mwezi Mei na kubeba mikanda yote minne ya uzito wa juu duniani kwa sasa na akiwa ni Undisputed (hajapoteza pambano lolote).

Kwa upande wa Anthony ametoka kushinda mapambano mawili mfululizo, huku akiwa na uwezekano wa kupigana kuwania mkanda wa IBF dhidi ya Daniel Dubois mwezi Septemba.

Wengine wanaofuatia kwenye orodha hiyo baada ya Fury ni Agit Kabayel, Zhilei Zhang na Efe Ajagba.

Related Posts