Na Mwandishi Wetu
UONGOZI wa Benki ya Biashara (TCB) umesema mali za benki hiyo ziliongezeka kutoka Sh.trilioni 1. 285 mwishoni mwa mwaka 2022 hadi kufikia Sh 1.389 mwishoni mwa mwaka 2023 ambalo ni sawa na ongezeko la Sh bilioni 103.9.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano Mkuu wa 32 wa mwaka wa Wanahisa benki hiyo na kufanya uwasilishaji wa taarifa ya fedha ya mwaka 2023 Mkurugenzi Mtendaji wa
TCB Adam Mihayo ametumia nafasi hiyo kueleza mafanikio ambayo benki hiyo imeyapata.
Akitoa taarifa kwa wanahisa hao amesema pia jumla ya mikopo yote iliongezeka kwa Sh bilioni 73.1, kutoka Sh bilioni 838 mwishoni mwa mwaka 2022 mpaka kufika Sh bilioni 911.2 Disemba 31, 2023 ikionyesha ongezeko la mwaka la asilimia 8.78.
“Ongezeko la mali lilichangiwa na ongezeko la amana za wateja ambazo ziliongezeka kwa asilimia 12.01 kutoka Sh trilioni 1 mwishoni mwa mwaka 2022 hadi kufika Sh trilioni 1.12 mwishoni mwa mwaka 2023.
Amefafanua katika mapato, TCB Benki ilishuhudia ongezeko kubwa la
mapato ya jumla kwa Sh.bilioni 19.27 sawa na asilimia 11.19 hadi kufika Sh. bilioni 192.1 ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo mapato yalikuwa Sh.bilioni 172.83 sawa na asilimia 1.72.
Pia Mapato ya riba yalichangia asilimia 79.61 ya mapato yote ya benki huku kiasi kilichobaki kikipatikana kutoka katika kamisheni, ada mbalimbali
na shughuli nyingine zilizofanywa na benki.
Amesema kupitia usimamizi wa kimkakati wa uwekezaji wake, Amana za TCB Benki katika benki nyingine zilishuka kwa Sh.bilioni 55.3 (asilimia 33.32), huku Amana za Serikali zikiongezeka kwa Sh bilioni 44.1 (asilimia 42.64), fedha taslimu na salio katika Benki Kuu ya
Tanzania (BOT) liliongezeka kwa Sh. bilioni 47.
Katika kipindi husika, Mihayo amesema walifanikiwa kuboresha mfumo wake wa kibenki kwa kuanzisha mradi unaowawezesha watumiaji wa mtandao wa Tigo kutoa hela zao katika mashine za ATM za benki hiyo.
Pia amesema majaribio ya mashine za ATM zinazowawezesha wateja kuweka fedha zao tayari yamefanyika, ambapo huduma hii inatarajiwa kuzinduliwa mwaka huu.
“Benki imenunua mfumo unaoratibu uhusiano wa benki na mteja wake (CRM system) ukilenga kutatua malalamiko
ya wateja kidigitali na kuwawezesha kujihudumia wenyewe
kupitia mobile banking.
“Sisi kama benki, dhamira yetu ya kudumisha ufanisi na kumridhisha mteja inatupa hamasa na uthubutu wa kujituma zaidi. Tunadhamiria kusikiliza na kuelewa mahitaji ya wateja wetu tukijua fika kwamba imani yao kwetu inazidi kuimarika.
” Tutaendelea kuhakikisha tunawawezesha kupata suluhisho la kifedha katika mahitaji yao
mbalimbali, ili kuchangia katika mafanikio ya Watanzania kama
ambavyo dhamira yetu ya kuwezesha ukuaji wa kiuchumi wa watu wetu inavyoeleza.”
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi, Martin Emmanuel Kilimba ameeleza kwamba wamejipanga kuendelea kuboresha ufanisi wao ili kuwezesha ukuaji wa taasisi hiyo