Dili la Mganda wa Azam lipo, Medo sasa ni Kagera Sugar

HUENDA Azam ikaachana na mpango wa kumsajili nyota wa Vipers ya Uganda, Yunus Sentamu kwa ajili ya msimu ujao.

Sentamu alikuwa katika mipango ya Azam msimu ujao, ingawa inaelezwa Kocha Mkuu, Youssouph Dabo amekuwa na imani kubwa na mshambuliaji mpya raia wa Colombia, Jhonier Blanco aliyefunga mabao 13, msimu uliopita akiwa na Fortaleza CEIF. 

KLABU ya Kagera Sugar iko katika mazungumzo na aliyekuwa Kocha wa Dodoma Jiji Mmarekani, Melis Medo kwa ajili ya msimu ujao. Kocha huyo wa zamani wa Coastal Union, kwa sasa yupo nchini baada ya kuondoka Dubai ambapo inaelezwa anaweza kujiunga na Kagera Sugar ambayo inatajwa huenda ikaachana na Kocha, Fredy Felix ‘Minziro’ anayewindwa na kikosi cha Geita Gold. 

UONGOZI wa Mashujaa umeanza mazungumzo ya kupata saini ya kiungo wa Dodoma Jiji, Rajab Seif Mgalula kwa ajili ya msimu mpya. Mgalula aliyecheza michezo 18 na kuasisti mawili, huenda akaondoka baada ya kocha Mkenya Francis Baraza kuondoka hivyo huenda kesho yake ikawa ngumu. Daudi Elibahati

KLABU ya Kagera Sugar imeanza mazungumzo ya kupata huduma ya beki wa Namungo na Taifa Stars, Abdulmalik Zakaria.   Zakaria aliyechezea timu mbalimbali ikiwemo Polisi Tanzania, inaelezwa anaweza akaondoka Namungo ili akapate changamoto mpya. 

BAADA ya vigogo wa soka kugongana kupambana kupata saini ya winga wa Alliance Girls, Mkenya Nelly Kache Simba Queens imeamua kuwaachia Yanga Princess dili hilo. Timu zote zilikuwa zikiwania saini ya winga huyo, lakini hadi sasa Yanga inaonekana kuwa siriazi na dili hilo baada ya kumrudia tena na kupeleka ofa kwa mchezaji huyo.

Related Posts