DKT. TULIA AWAONGOZA WAJUMBE WA IPU KUTEMBELEA VIVUTIO VYA ZANZIBAR

Rais wa umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameongozo Ujumbe wa kamati ya Uongozi ya Umoja huo kwa kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria na vivutio vya Utalii katika Mji Mkongwe Zanzibar leo tarehe 20 Juni, 2024.

Dkt. Tulia amesema kupitia ziara hiyo imeongeza chachu ya kuitangaza Zanzibar kupitia vivutio vyake kimataifa kwani wageni hao watakua Mabalozi wa kuutangaza utalii wa Zanzibar.

Akizungumzia kuhusiana na maazimio ya kikao kilichofanyika na Viongozi hao, amesema wamejadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na akili Mnemba, haki za Binaadamu, Demokrasia pamoja na upitishaji wa sera ya unyanyasaji wa kijinsia.

Kikao cha Kamati ya uongozi wa IPU kimefanyika visiwani Zanzibar hapo jana kwa ajenda ya kujiandaa na Mkutano Mkuu wa Umoja huo ambao umepangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.



Related Posts