Na Mwandishi Wetu
VIONGOZI mbalimbali wa Serikali wametembelea Banda la MSD kwenye maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo yanafanyika kitaifa mkoani Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 June, 2024.
Miongoni mwa viongozi waliotembelea ni Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo George Simbachawene ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na Ridhiwani Kikwete (Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Akizungumza akiwa katika banda hilo Waziri Simbachawene amesema anafurahishwa na namna MSD inavyotekeleza majukumu yake katika kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za afya “nimefurahishwa na namna MSD ilivyosambaza mashuka kwenye majimbo yetu ambayo yamesaidia katika utoaji wa huduma za afya”
Ameipongeza pia MSD kwa kupeleka haraka Jokofu la kuhifadhia miili Kituo cha Afya Kibakwe – Mpwapwa – Dodoma ambalo lilikuwa linahitajika kwa kiasi kikubwa.