Idadi ya vifo vya mama wajawazito vyapungua Manyara.

Idadi ya Vifo vya wanawàke wajawazito Mkoani Manyara imepungua kutoka vifo 49 mwaka 2022 hadi kufikia vifo 24 kwa mwaka 2024.

Hayo Yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa Wa Manyara Queen Sendiga wakati wa Kikao cha kutafuta uendelevu wa mfumo wa M MAMA Mkoani Hapo,Ambapo mfumo huu unatekelezwa na serikali kushirikiana wa wadau vodaphone foundation,Touch foundation na pathfinder international.

Sendiga amesema idadi hiyo huenda ikaongezeka kufikia mwishoni mwa mwakà 2024 kama hatua za haraka hazitachukuliwa Kudhibiti vifo hivyo ambapo kwanzia mwezi january hadi mwezi June vifo vya mama wajawazito vimefikia 24.

Aidha Queen sendiga ametoa Onyo kwa waganga wakuu wa wilaya na kutaka kupewa taarifa za kina kwa kila kifo cha mjamzito

“kila kifo Cha Mama mmoja kinapotokea ninahitaji kupata maelezo ha kutosha ya utaalamu,ni nini kimesababisha mama Huyo Akafa”

” Mganga Mkuu Na Timu yake na waliokuwa zamu wakati mama aliyefariki watupatie maelezo ya kina yatakayoturidhisha tuseme kuwa Mama huyu ilishindikana akapoteza maisha”Amesema Sendiga Mkuu wa mkoa wa Manyara

Related Posts