Polisi Morogoro wafanya ukaguzi magari ya shule

Jeshi la Polisi mkoa Morogoro limewataka wamiliki wa Magari yanayobeba wanafunzi (School Bus) katika kipindi hiki cha likizo kuhakikisha magari hayo kuwa ni mazima kwaajili ya matumizi ya wanafunzi mara tuu shule zitakapo funguliwa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ASP) Pascal Mwakabungu akiwa na timu ya ukaguzi wa magari alipokuwa akifanya Ukaguzi wa magari hayo ili kuthibitisha Ubora wakati shule zikiwa zimefunguliwa Juni 20, 2024

Aidha, ASP Mwakabungu amesema katika kipindi hiki cha likizo magari yote yanayotumika kubeba wanafunzi yanatakiw kufanyiwa ukaguzi na wakaguzi wa magari ili kubaini matatizo ya magari hayo na kuyarekebisha mapema ili kuendelea na huduma mara wanafunzi wanaporudi shuleni.

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Komba Hussein ambaye ni Mkaguzi wa Magari wa Jeshi la Polisi mkoa Morogoro amesema kuwa magari mabovu yanayo bainika yatatakiwa kufanyiwa marekebisho na hivyo zoezi hili ni endelevu kwaajili ya usalama wa watoto wetu

Related Posts