VODACOM OPEN LUGALO 2024 KUTIMUA VUMBI JULAI

MASHINDANO makubwa ya ‘Vodacom Open Lugalo 2024’ yanatarajiwa kutimua vumbi Julai 5,6 na 7 mwaka huu katika viwanja vya Lugalo, Dar es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa klabu wa hiyo, Bregedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo amesema mashindano hayo yatashirikisha klabu zote nchini.

Luwongo amesema wachezaji wameanza kujisajili kwa kasi kwa lengo la kuonyesha uwezo wao katika mashindano hayo.

“Mashindano haya yatashirikisha rika zote, pia maadhari ya uwanja watakuwa ya kipekee kutokana na ukubwa wao.”

Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Gilman Kasiga amesema wachezaji watakoshiriki mashindano hayo watapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

Ameeleza kuwa baada ya kumalizika kwa mashindano klabu ya Lugalo inatakiwa kuwasilisha ripoti ya fedha kwa TGU kama ilivyotakiwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro.

Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom, Aileen Meena amesema lengo la kudhamini mashindano hayo ni kuunganisha michezo na teknojia.

“Udhamini huu utakuwa endelevu pia kuanzisha Vodacom Gofu Tour kwa lengo la kukuza mchezo huu kimataifa”.

Related Posts