*Ni katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani Juni,25
Na Chalila Kibuda Michuzi TV,Bagamoyo
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) zimetoa elimu ya kwa Mabaharia pamoja kufanya usafi katika fukwe za bahari za Kaole na Dunda.
Akizungumza na Mabahari katika Bandari ya Bagamoyo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani ambayo Tanzania inafanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nianjema wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ,Afisa Mwandamizi wa Ukaguzi na Usajili wa Meli wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Gadaf Chambo amesema kuwa Manahodha wahakikishe vyombo vyao wanakuwa na vifaa uokozi pamoja na simu za upepo na kama wao wamiliki hawataki kuweka watoe taarifa Shirika hilo.
Amesema manahodha katika vyombo vyao wanapotea na wakati mwingine wanapotea maisha ni kutokana na kukosa vifaa vya uokozi.
Chambo amesema kuwa kupoteza maisha kuna gharaimu familia hivyo licha kufanya kazi kwanza ni kuangalia usalama.
Chambo amewataka mabaharia kuzingatia kuwa na vifaa vya uokoaji katika mitumbwi yao hasa wawapo katika sehemu yao ya kazi Baharini, ili kuokoa maisha yao inapotokea changamoto.
Mkurugenzi wa Mamlaka Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) Mtumwa Said Sandali amesema kuwa watumiaji wote wajisajili na kuwa leseni katika kurahisha Serikali mbili ziweze kutoa huduma.
Sandali amesema kuwa serikali inawategemea kutoka ana na kuwa na mchango katika uchumi wa nchi.
Kwa upande wa usafi Mwenyekiti Usimamizi wa Fukwe Nuru Tamimu amesema TASAC na ZMA mmeonyesha kujali mazingira ya bahari pamoja na kushiriki usafi.
Amesema kuwa wakiwa wasimamizi wa fukwe wanashukuru kutumia maadhimisho kufanya usafi
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) Mtumwa Said Sandali akitoa elimu kwa Manahodha wa Vyombo Vidogo Majini na Wavuvi katika kuelekea Maadhimisho ya Mabaharia Duniani Juni 25 katika Bandari ya Bagamoyo.
Afisa Mkaguzi na Msajili wa Meli wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Captain Gadaf Chambo akitoa elimu kwa Manahodha na Wavuvi juu ya matakwa ya kisheria usajili wa vyombo pamoja vifaa vya uokozi W katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani Juni 25.
Picha mbalimbali za matukio ya Usafi katika Fukwe za Kaole na Dunda