NYOTA wa Simba aliyekuwa akikipiga kwa mkopo Mtibwa Sugar, iliyoshuka daraja, Jimmyson Mwanuke amedaiwa kuanza mazungumzo na Mashujaa kwa ajili ya kuitumikia kwa msimu mpya.
Mwanuke aliyekuwa akitumika Simba kama kiraka, akimudu zaidi kucheza kiungo mshambuliaji, lakini wakati mwingine akitumikishwa kama beki ameshamaliza mkataba aliokuwa nao na Simba iliyomtoa kwa mkopo kwa Mtibwa katika dirisha dogo lililopita na kwa sasa inalezwa mazungumzo yake na Mashujaa yapo mahali pazuri.
Nyota huyo ni kati ya wachezaji wengi walioshuka na Mtibwa ambao wanadaiwa wapo mbioni kutimika katika timu hiyo na kabla ya kutua Simba aliwahi kukipiga Gwambina iliyocheza Ligi Kuu kabla ya kufutika baada ya kuadhibiwa na TFF.