· Ni Mkongo wa Mawasiliano baharini wenye uwezo mara10 zaidi ya iliopo
· Kumaliza changamoto ya kukosekana kwa huduma ya intaneti kutokana na sababu ya kukatika kwa mkongo wa baharini
· Uchumi wa kidijitali unatarajiwa kukua kwa kiwango cha juu zaidi
KAMPUNI ya Airtel Tanzania imeanza kutumia rasmi Mkongo wa mawasiliano unaopita baharini wa 2Africa wenye urefu wa kilomita 45,000 ukiunganisha mabara matatu ili kutoa huduma za intaneti ya kasi zaidi, jambo litakaloleta maendeleo makubwa katika kupanua na kuimarisha miundombinu ya kidijitali nchini Tanzania.
Mkongo huu wa kisasa wa 2Africa unaopita chini ya Bahari na kusimamiwa na Airtel Tanzania utaiweka Tanzania katika viwango vya juu vya mabadiliko ya kukua kwa huduma za kidijitali, na kukidhi mahitaji ya uchumi wa nchi unaoendeshwa na huduma za mtandao (data).
Mkongo wa 2Africa sasa umeanza rasmi kuhudumia makampuni ya teknolojia ambayo sasa yanapokea masafa ya uwezo wanaohitaji kupitia kituo cha Airtel Cable Landing Station kilichopo Dar Es Salaam Mbezi Beach, Kilichozinduliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkongo mpya wa Airtel 2Africa unakuwa suluhisho la pekee na ulinzi wa mikongo au kebo zingine za mawasiliano zinazopita chini ya bahari nchini. Uzinduzi huu wa Airtel Tanzania umekuja wakati muafaka, hasa kutokana na kukatika kwa nyaya za mkongo wa mawasiliana unaopita chini ya bahari hivi karibuni ambazo ziliathiri baadhi ya maeneo ya Afrika Mashariki, ikiwemo Tanzania.
Mkongo wa mawasiliano wa 2Africa unaozinduliwa sasa unauwezo wa kusafirisha masafa mara 10 zaidi ya ile iliyopo na itasaidia kuanzishwa kwa vituo vya kuhifadhi kumbukumbu kieletroniki (Data centres) ili kukidhi ongezeko la shughuli za kidijitali nchini.
Kuwashwa kwa Mkongo wa 2Africa kunaleta manufaa makubwa katika kuikuza Tanzania ya ya kidijitali kutokana na kuboreshwa kwa matumizi ya mtandao katika uhamishaji wa maudhui na kuhakikisha kasi ya juu ya 4G na 5G kwa watumiaji. Mkongo wa mawasiliano wa 2Afrika inaiunganisha Tanzania na maeneo 43 duniani, na inahudumia zaidi ya watu bilioni 3 na kukuza muunganiko wa kimataifa wa wafanyabiashara kidijitali.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alizindua kituo cha Mkongo wa mawasiliano baharini – Airtel Cable Landing Station kinachotua Dar Es Salaam maeneo ya Mbezi beach ambapo pia alizindua mtandao wa 5G wa Airtel Tanzania Tukio lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Pamoja na Rais Mstaafu Mh. Jakaya Kikwete. Alisisitiza kuwa mkongo huo utaleta mabadiliko chanya ndani ya sekta ya mawasiliano katika kuboresha uchumi wa Tanzania kupitia huduma bora kidijitali.
“Kuzindua Kituo cha 2Africa Cable landing Station kunaashiria hatua muhimu na mustakabali wa nchi yetu kupaa kidijitali.. Miundombinu hii sio tu italeta mapinduzi katika huduma za mawasiliano lakini pia itaharakisha ukuaji wa Uchumi kwa kuimarisha muungano na mataifa mengine,” Rais Hassan alisema.
Kituo cha Airtel 2Africa ni muhimu katika kumaliza changamoto ya mgawanyiko wa kidijitali iliyopo barani Afrika na kwa kupitia, Mkongo huu, Tanzania itafanikiwa kuendeleza biashara ya mtandaoni na utawala wa kidijitali. Mkongo huu unaunga mkono mipango ya Wizara ya Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari, ikiwemo mipango ya maabara ya akili mnemba na maabara za roboti.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Dinesh Balsingh, alisisitiza kwamba mazingira wezeshi ya serikali katika kupatikana kwa leseni pamoja na uwepo wa mfumo bora wa udhibiti nddio sababu zilizowezesha Airtel Tanzania kuzindua kituo chao cha Airtel 2Africa kabla ya nchi nyingine. Alieleza kuwa Tanzania inashuhudia kuwashwa kwa mkongo wa 2Africa na kuanza kugawa masafa yenye uwezo wa juu moja kwa moja sasa.
“Ujio na uwepo wa Mkongo wa mawasiliano wa baharini wa 2Africa umefanikiwa kuwa nchini Tanzania kutokana na maono ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suhuhu Hassan na Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya habari, Nape Nnauye. Mkongo wa 2Africa unaifanya Tanzania kuwa kitovu na lango la kusambaza huduma kidijitali kimataifa, kukuza fursa za kiuchumi na maendeleo ya kiteknolojia. Mpango huu utatoa huduma na uwezo wa hali ya juu wa mtandao kwa watumiaji kadri maudhui yanavyoratibiwa na kuhamishwa popote, katika kuikuza Tanzania ya Kidijitali,” alieleza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk.Jabiri Bakari alisema kuwa Mkongo huu mpya wa mawasiliano wa 2Africa unaopita baharini utachochea na kuboresha zaidi huduma bora za intaneti nchini.
“Mkongo huu mpya utakuwa msaada mkubwa katika kukabiliana na mhitaji ya huduma za mtandao wa intaneti nchini, ambazo mahitaji yake yamekuwa yakioongezeka maradufu kila baada ya miaka miwili. Nina hakika kuwa teknolojia hii itapelekea utekelezaji wa haraka wa mkakati wetu wa kuhimiza matumizi ya TEHAMA katika sekta zote na kuboresha uchumi wa kidijitali ambao Tanzania inatamani kufikia,” alisema Dk. Bakari.
Hotuba ya Waziri wa Mawasiliano MheshimiwaNape Nnauye wakati wa uzinduzi wa kituo cha Airtel 2Africa, alisema uwepo wa Mkongo wa 2Africa utasaidia kuunganisha nchi kimataifa na kuwepo kwa mifumo ya kibunifu kidijitali ikiwemo kuunganisha mifumo mbalimbali ya serikali kuwa jumuishi.
“Mkongo wa 2Africa utaleta maendeleo kwa huduma za mawasiliano katika nchi yetu na kuwa kivutio na suluhisho la mawasiliano kidigitali kwa nchi za Afrika Mashariki,” alisisitiza.
Kulingana na makadirio ya RTI International, Mkongo wa 2Africa unatarajiwa kuzalisha kati ya USD 26.4 bilioni na USD 36.9 bilioni ikiwa ni matokeo ya ukuaji kiuchumi kutokana na huduma zitakazotolewa na mkongo huu barani Afrika ndani ya miaka ya awali.
Kwa kupitia Mkongo wa mawasilino chini ya bahari wa 2Africa, Airtel Tanzania inazidi kuwawezesha Watanzania kufurahia kasi na uwezo wa juu ya mtandao na kufikisha huduma kwa watanzania waliopo mjini na vijini kote.
MUHIMU:
Kwa kampuni ya Techolojia yanazohitaji huduma za mtandao wa intaneti yenye uwezo zaidi toka katika kituo cha 2Africa anaweza kuwasiliana na Airtel Tanzania kupitia enterprisesoulution@airtel.co.tz au wasiliana na Yassin Hemed kwa namba +255 784 670 055.