Cheki ‘SUB’ ya kadi nyekundu kikapu

KATIKA kila mchezo kuna raha yake kwa mashabiki na hata wachezaji.

Lakini, linapokuja suala la wachezaji kuingia mchezoni kutokea benchi (sub), kwenye kikapu kuna maajabu zaidi kwani mchezo yeyote anaweza kuingia uwanjani ili mradi tu awe katika benchi la nyota wa akiba.

Kwenye soka na michezo mingine mingi, mchezaji anapopewa kadi nyekundu sheria za michezo hiyo haziruhusu kuingia mchezaji mwingine na hii ndiyo tofauti na kikapu akitolewa mchezaji ndani ya uwanja anaingizwa mwingine.

Kwa upande wa mchezo wa kikapu mchezaji anayetolewa nje ya uwanja wao wakiita ‘disqualification’ ni mchezaji aliyefanya madhambi makubwa yakiwemo ya kuhatarisha hali ya kimwili dhidi ya wenzake au kupigana.

Baada ya mchezaji kufanya tukio na kutolewa, mwamuzi ananyoosha mikono miwili juu akiwa amekunja ngumu akiashiria atolewe nje ya uwanja na adhabu yake ni ya kutoruhusiwa kukaa kwenye benchi la wachezaji wa akiba kwenye mchezo husika.

Hata hivyo sheria ya mchezo huo inaeleza kwamba anaruhusiwa kucheza mchezo unaoufuata tofauti na soka adhabu ni kukosa michezo kadhaa kulingana na kanuni.

Katika mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), hakuna tukio lolote lililotokea kwa mchezaji kutolewa nje ya uwanja.

Issa Salumu, kocha wa kikapu kutoka Temeke, alisema mchezo wa kikapu unatumia akili nyingi na siyo wa vurugu, hivyo uungwana unatawala zaidi

“Ukiona mchezaji wa kikapu anapigana ni mchezaji aliyeshuka kiwango cha uchezaji tofauti na mchezaji anayeinukia katika mchezo huo,” alisema Salumu.

Related Posts