UONGOZI wa Simba unafuatilia kwa ukaribu huduma ya beki wa kati wa kimataifa wa DR Congo, Nathan Idumba Fasika anayechezea Klabu ya Valerenga ya Norway.
Fasika anayeichezea Valerenga kwa mkopo akitokea Cape Town City ya Afrika Kusini, inaelezwa kwamba tayari mabosi wa Simba wanafukuzia saini yake huku wakiamini kwamba atakuwa ni mbadala sahihi wa beki Mkongomani mwenzake, Henock Inonga anayesemekana kwamba huendea akatua katika timu ya FAR Rabat ya Morocco.
Tayari Simba imeanza mchakato wa kumsajili beki huyo baada ya dili la kumuuza Inonga kufikia pazuri, hivyo fedha zitakazotumika katika mauzo hayo wanatarajia kuzitumia kushusha kifaa kipya ambacho huenda ikawa ni mchezaji huyo.