Urusi yaishutumu Marekani kuhusika na shambulizi la Crimea – DW – 24.06.2024

Akinukuliwa na Shirika la TASS, Msemaji wa serikali ya Urusi, Dmitry Peskov amesema wanajua dhahiri nani hasa ambae amehusika na shambulioa hilo, nani aliyelengwa na makombora hayo ya teknolojia ya kisasa na kwamba si Ukraine ambayo imehusika katika shambulio hilo.

Bila kupindisha kauli msemaji huyo aliinyoshea kidole Marekani kwa kile alichokisema kuhusika moja kwa moja katika operesheni hiyo ambayo imesababisha raia kupoteza maisha, jambo ambalo haliwezi kufumbiwa macho na taifa lake.

Urusi: Majibu wa shambulizi ni suala la muda

Sevastopol kwenye Rasi ya Crimea
Eneo lililoshambuliwa la mji wa pwani wa Sevastopol huko CrimeaPicha: Sergei Malgavko/TASS/dpa/picture alliance

Msemaji huyo aliongeza kwa kusema kwamba muda utatoa majibu ya hatua itakayochukuliwa na Urusi. Kufutia shambulio la mji wa Crimea wa Sevastopol la Jumapili Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi pia imemwita balozi wa Marekani mjini Moscow, Lynne Tracy kwa mahojiano.

Ikulu ya Urusi-Kremlin inadai Washington haitoi tu silaha kwa Kiev lakini pia wataalamu ambao wanasaidia kusimamia ufyatuaji wa makombra ya masafa marefu kwa ustadi.

Dagestan yatangaza siku tatu za maombolezo

Katika hatua nyingine huko katika mkoa wa kusini wa Urusi wa Dagestan kumetangazwa siku tatu za maombolezo, baada ya mauwaji ya watu 20 kulikofanya na wapiganaji wenye itikadi kali. Wengi wa waliuwawa ni polisi katika kile kinachotazamwa kama mashambulizi ya kupangwa katika miji miwili tofauti.

Nje ya taifa hilo Umoja wa Ulaya umeidhinisha mpango wa kutumia awamu ya kwanza ya faida iliytokana na mali za Urusi zilizozuliwa kwa msaada wa kijeshi kwa Ukraine,ikiliweka kando pingamzi la Hungary katika hatua hiyo.

Soma zaidi: Umoja wa Ulaya waridhia vikwazo vipya dhidi ya Urusi

Katika hatu za mapema ya leo, mkuu wa sera za kigeni wa wa Umoja wa Ulayxa Josep Borrell alitangaza kuwa umoja huo umebaini njia ya kutumia fedha hizo kununua silaha na misaada mingine kwa Ukraine bila kuhitaji ridhaa ya Hungary. Awamu ya mwanzo ya faida  ambayo ni karibu Euro bilioni 1.4 inatarajiwa kuwa tayari kwa matumzi juma lijalo.

Vyanzo: DPA/AP

 

Related Posts