Wanawake msisahau majukumu yenu ya kutunza familia.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Batlida Buriani amewataka wanawake mkoani hapa licha ya kushirikisha kwenye shughuli za kujitafutia kipato wahakikishe hasahau jukumu la malezi kwa watoto wao.


Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo Kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia Kwa watoto katika wilaya mbalimbali za mkoani huu jambo ambalo lina haribu ustawi wao wa ukuzaji .

Rai hiyo ameitoa jana wakati akizindua msimu wa nane wa maonyesho ya wajasiriamali wanawake ya Tanga women gala alisema kuwa ni muhimu kutoweka kando jukumu la malezi kwani ni sehemu ya wajibu wao mkubwa.

“Kama tunavyojua jukumu la malezi ya familia ni la mwanamke hivyo shughuli za kujitafutia kipato lisisababishe tukasahau jukumu hilo muhimu Ili kuwalinda watoto wetu na kufanyiwa vitendo vya ukatili na watu wenye Nia ovu”alisema RC Buriani.

Alisema kuwa Hali sio nzuri kwa katika mkoa huo kutokana na kuwepo na vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo aliwataka wanawake kukemea matendo hayo lakini na kurudi kujikita katika malezi kwa watoto wao.


Aidha aliwataka wanawake hao wajasiriamali kuhakikisha wanajikita katika kuzalisha bidhaa zenye ubora ambazo zitaweza kuleta ushindani katika soko na hivyo kuweza kuleta maendeleo ya kiuchumi kwao na mkoa huo Kwa ujumla.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Tanga woman gala Latifa Makau alisema kuwa Maonyesho hayo yamekuwa ni tija ya kuibua fursa lukuki kwa wajasiriamali hao wanawake na hivyo kusaidia kuchangia uchumi wao lakini na mkoa Kwa ujumla.

“Tumekuwa tukitumia maonyesho haya sio tuu kutangaza bidhaa za wanawake Bali kutoa elimu Kwa wajasiriamali hao kuhusu huduma mbalimbali ikiwemo za mikopo ,akiba sambamba na uwekezaji”alisema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo alisema kuwa kupitia maonyesho hayo wanawake wa Tanga wamekuwa wakiongea hamasana muamko wa kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi mwaka hadi mwaka .

“Maonyesho haya yamekuwa na tija kwetu waandaji kwani licha ya kutambua mchango wa mwanamke katika uchumi lakini Sasa tunakwenda kujenga uchumi imara Kwa mwanamke Kwa kumbainishia fursa zilizopo katika kushiriki kwenye ukuwaji wa uchumi wa Taifa hili”alibainisha Makau.
[12:56, 25/06/2024] Geena Tza: okay

Related Posts