MSONDE ATAKA UFUATILIAJI UFUNDISHAJI SOMO LA KINGEREZA

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde amewataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kufuatilia kwa karibu maendeleo ya Elimu Msingi hasa ufundishaji wa somo la kingereza ili kuhakikisha wanafunzi wanapata ujuzi na umahiri katika lugha ya kingereza.

Dkt. Msonde amesema hayo kwenye kikao kazi cha majumuisho ya ziara ya katika mkoa wa Mara kilichowakutanisha walimu,walimu wakuu,wakuu wa shule,Maofisa Elimu na wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Mara kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa.

“Nadhani mnaona yanayoendelea katika shule zetu mfano mtoto anamaliza darasa la saba na amepita shule ya msingi kote hajui kingereza sasa na sisi viongozi tusione jambo hilo kama la kawaida na kule kwetu walimu wanaishia kusema ni shule ya serikali kwahiyo najiuliza kuna mtaala wa serikali na binafsi? lakini kule kwenye binafsi walimu ni walewale wamesoma vyuo vilevile na watoto wanafundishwa mwaka mmoja wanajua kingereza lakini huku kwetu wanasema ya serikali, uzuri walimu wa Tanzania wana juhudi na wanajituma sana kwahiyo tulikuwa tunajaribu kuwaonesha wafanyeje ili tutoke hapo tutoke” amesema

Akisisitiza kuhusu ufuatiliaji huo Dkt. Msonde amewataka wasimamizi wa Elimu ngazi ya kata,Halmashauri na Mkoa kuhakikisha maelekezo yote ya kubadili mtazamo wa walimu yanafika kwa walimu wote na ifikapo mwisho wa muhula wa pili wa masomo wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wawe wamepata ujuzi na umahili wa lugha hiyo ikiwa ni pamoja na kuongea,kusoma.

Ziara ya timu ya Elimu kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI ikiongozwa na Naibu Karibu Mkuu Dkt. Charles Msonde imehitimishwa rasmi katika mkoa wa Mara ikiwa tayari imefika katika mikoa yote ya Tanzania Bara ili kupisha maandalizi ya Mhula wa Pili unaotarajiwa kuanza Julia 01,2024.

Related Posts