Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko (watatu kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mawasiliano na Masoko wa Hospitali ya Kairuki, Elvin Eliezer (kulia), kuhusu huduma za upimaji afya bure zinazotolewa kwa wakazi wa Ubungo alipotembelea banda la kutoa elimu ya kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Magufuli jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto ni Meneja wa NHIF Mkoa wa Kinondoni, Dk. Raphael Mallaba. (Na Mpiga Picha Wetu).
Menaeja wa ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Dr Raphael Mallaba akiwataka Wananchi kupokea elimu ya kujua faida na umuhimu wa kujiunga na bima ya afya ikiwa ni fursa kama fursa nyinginezo kwa kufikwa na maofisa kwenye maeneo wanayofanyia shughuli zao za kiuchumi,wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya elimu ya bima ya afya mtaani kwako kwenye viwanja vya stendi ya Magufuli jijini Dar es Salaam,pembeni kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Hassani Bomboko ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Msimamizi wa ofisi ya Wilaya ya Ubungo Bi Jane Mukoba (CPA T) akitoa taarifa fupi ya mafanikio kwa mgeni rasmi.