TETESI ZA USAJILI BONGO: Ibrahim Abraham awindwa Pamba Jiji

BAADA ya kutangaza kuachana na mastaa wao walioipandisha timu hiyo, uongozi wa Pamba Jiji FC unawinda saini ya Ibrahim Abraham.

Beki huyo wa kushoto wa Tanzania Prisons ambaye anamudu kucheza nafasi tatu uwanjani yupo kwenye hatua nzuri za kukamilisha dili hilo kwa mkataba wa miaka miwili.Charity James

BEKI wa kati, Ismail Mgunda aliyemaliza mkataba na Ihefu FC ambayo haijaonyesha dalili ya kuhitaji huduma yake msimu ujao, dili lake liko mbioni kukamilika Mashujaa na kama makubaliano kati ya pande hizo mbili yatakamilika basi msimu ujao atakuwa ndani ya maafande hao.

Mchezaji huyo aliwahi kuichezea Ruvu Shooting vipindi viwili tofauti, Jomo Cosmos na msimu uliopita alikuwa akiitumikia Ihefu Fc.

BEKI wa zamani wa Kagera Sugar, Abdallah Mfuko yupo kwenye mazungumzo ya kusaini mkataba na JKT Tanzania wanaopambana kusuka kikosi bora baada ya kuponea kushuka daraja.

Mfuko anamudu kucheza vizuri eneo la beki wa kati na amekuwa akitumika zaidi eneo hilo kwenye timu zote alizowahi kuzitumikia.

KAMA ilivyo kwa misimu miwili iliyopita, Yanga Princess imepanga kuachana na wachezaji nane wa kikosi hicho. Hadi sasa inaelezwa wachezaji sita wa kigeni akiwemo Madina Traore na mzawa Lucy Mrema ni miongoni mwa majina ambayo yataondolewa kikosini hapo.

BAADA ya kumaliza mkataba wake na Namungo, kipa mkongwe, Deogratius Munishi ‘Dida’ anawindwa na Ken Gold ili kuongeza nguvu kwenye kikosi cha timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu.

Dida inatajwa uzoefu wake utaisaidia timu hiyo kuonyesha ushindani katika ushiriki wao wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara msimu ujao.

KIUNGO wa Mlandege FC, Abdallah Kulandana ameingia kwenye rada za timu za Ligi Kuu Bara akihusishwa kujiunga na Kagera Sugar na KenGold.

Kiungo huyo mkabaji ambaye amewahi kukipiga JKU na Kundemba FC, amekiri kuwa kwenye mazungumzo na timu tano za Ligi Kuu Bara na hawezi kuziweka wazi hadi dili litakapokamilika.

JANET Matulanga ni miongoni mwa majina ya wachezaji watano wanaojadiliwa na JKT Queens kwa ajili ya msimu ujao.

JKT imevutiwa na kiungo huyo wa ushambuliaji anayekipiga Ceasiaa Queens kutokana na uwezo wake wa kufumania nyavu akiweka kambani mabao saba.

Related Posts