VIJANA WENYE BUNIFU MBALIMBALI TANGA KUPATIWA FURSA ZA RUZUKU


Mwakilishi wa Shirika la Botnar Foundation Philotheusy Mbogoro akizungumza wakati akifungua mafunzo maalumu ya ufundi na Udereva wa Bajaji za Mfumo wa Umeme yaliyoanza leo kwenye Shule ya Sekondari Tanga School ambapo vijana zaidi ya 40 wanapata mafunzo hayo.

Mmoja kati ya Washirika na Wafanyakazi wa Tanzania Open Innovation Organization na Robotech Abdulwahab Issa akizungumza wakati akifungua mafunzo maalumu ya ufundi na Udereva wa Bajaji za Mfumo wa Umeme yaliyoanza leo kwenye Shule ya Sekondari Tanga School ambapo vijana zaidi ya 40 wanapata mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein akizungumza na baadhi ya madereva Bajaji wakati wa mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein akizungumza na baadhi ya madereva Bajaji wakati wa mafunzo hayo

Afisa Vijana Jiji la Tanga Fadhili Secha kulia akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo

Na Oscar Assenga, TANGA.

VIJANA wanaofanya shughuli za Ubunifu Jijini Tanga wamewekewa bayana uwepo wa mambo mazuri kwao ikiwemo fursa za kupatiwa ruzuku ili waweze kufanya bunifu ambazo zinaweza kuwaingiza wenzao kwenye ajira na maisha bora zaidi.

Hayo yalisemwa leo na Mwakilishi wa Shirika la Botnar Foundation Philotheusy Mbogoro wakati akifungua mafunzo maalumu ya ufundi na Udereva wa Bajaji za Mfumo wa Umeme yaliyoanza leo kwenye Shule ya Sekondari Tanga School ambapo vijana zaidi ya 40 wanapata mafunzo hayo.

Alisema kwamba kupitia Tanga yetu ipo kwa ajili ya kusaidia vijana wenye ubunifu mkoani humo kwa ajili ya kuwawezesha kunufaika kupitia Taasisi mbalimbali ikiwemo TOIO, Project Inspire Sterm Park na wengine wanawawezesha bajeti ya kuweza kuwasaidia.

Kati ya vijana hao 35 ni kutoka chuo cha Ufundi Veta na wengine ni kutoka mitaani wenye kutakuja kuwa ufundi wa Bajaji ambapo mafunzo hayo yanaendeshwa na Kampuni ya Robotech Labs kwa kushirikiana na Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization chini ya ufadhili wa Tanga Yetu.

Mafunzo yaliyotolewa ni namna ya kuweza kutumia vyombo hivyo kwa urahisi, ufungaji ikiwemo uunganishaji wa bajaji kwa kila sehemu kabla ya kukamilika na kuwa chombo kamili ambayo itawasaidia kujua hata jinsi ya kufanya marekebisho yake.

Alisema kwamba wao wanawasaidia kupata ruzuku hizo ili kuwawezesha vijana wengi waweze kutumia fursa zilizopo Jijini Tanga na kuweza kujikwamua kiuchumi.

Alisema vijana hao wanapaswa kutumia fursa hizo zilizopo ikiwemo kujitahidi kuwa wabunifu na wasilale kutokana na uwepo wa vitu vingi vya kufanya ambavyo vinaweza kuwaondoa kukaa kijiweni kutokana na kukosa kitu cha kufanya.

Aidha alisema umuhimu wa mafunzo hayo yanatoa fursa kwa vijana wengi kuweza kupata ujuzi wa kuweza kuwasaidia kujiajiri na kufanya shughuli zao ziwe bora kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo ufungaji wa samaki, uvuvi, kilimo, ufungaji wa kuku hivyo wanawataka vijana kuwa mabalozi wazuri kujifunza

Akizungumzia mafunzo ya Bajaji za umeme alisema kwamba zinawapa fursa ya kuunganisha bajaji za umeme ambazo wanaweza kupata biashara ya kuziunganaisha, kufanya matengenezo, vituo vya kuzifanya marekebisho.

“Lakini pia zinatoa fursa wengine kuchaji, kuziuza na fursa za ajira ambazo zinakwenda kwa vijana ni wengi kupitia bajaji na pikipiki za umeme zinazokuja na hata magari umeme kwa hiyo wamekuwa kuwa na teknolojia hiyo uwezo mkubwa wa kukamata biashara ya kuhudumia bajaj,pikipiki na hata magari ya umeme itakuwa mikono mwenu hivyo mzingatie mafunzo haya”Alisema

Awali akizungumza katika mafunzo hayo ni Mmoja kati ya Washirika na Wafanyakazi wa Tanzania Open Innovation Organization na Robotech Abdulwahab Issa alisema kwamba wapo kwenye mafunzo ya bajaji wao waona namna gani bajaji zinazounganishwa zikiwa zimetoka kutoka kiwandani.

Alisema pia waweze kuona mifumo ya umeme na mota vinavyofanya kazi lengo kubwa na mahususi vijana hao waweze kuona na kupata uelewa namna vyombo hivyo vinavyoweza kufanya kazi na wao jinsi gani ya kuweza kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku na kuokoa kipato.

Alisema bajaji hiyo inaweza kutembea kwa umbali wa kilomita 80 mpaka 100 kwa kutumia chaji ya asilimia 100 kwa bajaji iliyochajishwa kwa sh 3000 hivyo inaweza kuokoa kipato cha matumizi kuokoa mafuta kuhamia huko kwa sababu ya masuala ya kimazingira.

Awali akizungumza katika mafunzo hayo Afisa Vijana Jiji la Tanga Fadhili Secha alisema wamekuwa wakishirikiana na vijana na wadau wa maendeleo kuwatumia vijana kutoka sehemu mbalimbali kuwaunganisha na wadau kuweza kupata vitu mbalimbali vinavyoendelea na Ubunifu wa Teknolojia.

“Ujio wa Bajaji za Umeme hapa vijana wamepata fursa muhimu kwa sababu ni teknolojia mpya ni itawasaidia kuepukana na gharama kubwa kuepukana na matumizi ya petroli ambayo ni gharama na kuweza kupata faida”Alisema

Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Bajaji Mkoa wa Tanga Rahim Makange alisema bajaji za umeme ni fursa kubwa kwa vijana wa Jiji hilo na wamepata elimu nabajaji hizo zinarahisisha mambo mengi na hazina gharama kutokana na kwamba gharama zake ni umeme hakuna kuingia sheli.

Alisema kwamba wameelewa umbali betrii ikichajiwa ikijaa inaweza kutoka Jijini Tanga hadi Korogwe kwa kuchaji lakini petroli ingekuwa ni gharama kubwa na hiyo itawaondolea ugumu wa maisha hivyo vijana wachangamkie fursa hiyo muhimu.

Related Posts