Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma.
Serikali
imesema kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa sasa inaendelea na hatua
ya utafiti wa uanzishwaji wa matumizi ya Sarafu za Kidijitali za Benki
Kuu (Central Bank Digital Currency) hapa nchini.
Hayo
yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad
Hassan Chande (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni, Mhe
Dkt.Faustine Engelbert Ndugulile, aliyeuliza Serikali ina mpango gani wa
kuanza kwa matumizi ya Sarafu za Kidijitali (Central Bank Digital
Currency) hapa nchini.
Mhe.
Chande alisema kuwa Benki Kuu imebaini kwamba, kama ilivyo kwa mataifa
mengi, uanzishwaji wa Sarafu za Kidijitali za Benki Kuu (Central Bank
Digital Currency), unahitaji kuanzishwa kwa uangalifu na umakini bila
kuleta athari hasi katika mifumo ya malipo iliyopo nchini na pia kuweza
kutatua tatizo halisi la malipo ambapo kwa sasa bado mifumo iliyopo
nchini inakidhi hali halisi ya uwezeshaji mwananchi kutuma fedha na
kufanya malipo.
‘‘Soko
letu bado linahitaji kuendelea kuboreshwa katika kuimarisha mifumo
iliyopo kwa kutumia vyanzo vinavyopatikana kwa urahisi na wananchi wengi
(simu za kawaida) tofauti na matumizi ya Sarafu za Kidijitali
zinazoitaji matumizi ya simu janja (smartphones),’’ alisema Mhe.
Chande.
Mhe.
Chande alisema kuwa nchi nyingi ikiwa ni pamoja na majirani zetu na
ukanda wetu bado wapo katika hatua hizi za awali za utafiti na kuboresha
mifumo ya malipo iliyopo.
wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema kuwa Serikali
inaendela na utafiti kuhusu matumizi ya fedha za kielektroniki kuangalia
namna nchi inaweza kunufaika endapo itahamia kwenye matumizi ya fedha
za mfumo huo wa kielektroniki.
unaendelea na sasa wanaangalia uzoefu katika mataifa ambayo yameanza
kutumia fedha za kidigitali ikiwemo Nigeria na nchi za Asia na baada ya
kukamilika hatua zitafuata kwa utaratibu unaofaa,’’ alifafanua Dkt.
Nchemba.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akitoa ufafanuzi kuhusu uanzishwaji wa
matumizi ya Sarafu za Kidijitali, bungeni jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe.
Hamad Hassan Chande (Mb), akijibu swali kuhusu uanzishwaji wa matumizi
ya Sarafu za Kidijitali, bungeni jijini Dodoma.