COSOTA WAISHUKURU MAHAKAMA, KESI KWENDA VIZURI

Afisa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Usuluhishi Tanzania (COSOTA), Dorine Sinare akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la mafunzo wa Wadau wa mahakama na wengine kuhusiana na Hati miliki na alama za biashara kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Saalaam.
OFISI ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kama wadau wakubwa wa haki miliki wanaipongeza Mahakama ya Tanzania kwa jitihada zake za kuhakikisha wanataoa mafunzo ya haki bunifu na alama za biashara kwa majaji na mahakimu wa mahakama kuu, za rufaa na mahakama zote nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 26, 2024, Afisa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Usuluhishi Tanzania (COSOTA), Dorine Sinare baada ya Mafunzo ya haki miliki na alama za biashara kufunguliwa na Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma. “Nashukuru Mahakama na Shirika la hakimiliki bunifu duniani (WIPO) kwa jitihada za kutoa mafunzo haya na kuwafikia watanzania.”
Amesema COSOTA, imesema mafunzo hayo ni muhimu kwasababu kulikuwa na ukiukwaji wa haki miliki, kuzulumiwa haki kimziki, kwenye filamu, kwenye vitabu, kwenye sanaa za ufundi, softwere zinazotengenezwa sasa anaweza kupeleka Mahakamani.
Amesema mahakama kupata mafunzo maana yake kesi zitakwenda vizuri na wadau watanufaika na kupata haki zao kupitia mahakama zilizopo hapa nchini.
Kongamano hilo la siku mbili limehudhuriwa na watendaji mbalimbali wa mahakama zaidi ya 200 pamoja na wadau wengine.

Related Posts