WADAU TANZANITE WAMPONGEZA SAITOTI – MICHUZI BLOG

Na Mwandishi wetu, Mirerani

WADAU wa madini wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wamempongeza Mkurugenzi wa kampuni ya GEM & Rock Venture, Joel Saitoti kwa kufanya mnada wa madini kwenye eneo hilo hivyo kuwanufaisha kiuchumi.

Kampuni ya GEM & Rock imeendesha mnada wa kuuza madini ya Tanzanite kwa wachuuzi wenye leseni kwenye kituo cha Tanzanite Magufuli, ndani ya ukuta unaozunguka migodi hiyo.

Mdau wa madini, Kaanael Minja amesema mnada huo umefanyika kwa kutenda haki kwani kuna baadhi ya watu wengi wasio na leseni ila wamebebwa na wenye leseni.

“Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu minada kama hii kufanyika na tunampongeza Saitoti kwa kuendesha mnada huu ambao utawanyanyua wengi kiuchumi,” amesema.

Mdau mwingine, Christian Salum amesema minada ya madini ikifanyika kila mara itawanyanyua kiuchumi hadi wachuuzi.

“Tunampongeza mkurugenzi wa kampuni ya GEM & Rock, Joel Saitoti kwa kuendesha mnada wa madini ya Tanzanite kwani watu wengi wamefaidika kiuchumi hivyo wengine waige hili,” amesema.

Mwenyekiti wa chama cha mabroka nchini, Jeremia Kituyo amesema kupitia mnada huo watu wengi wamenufaika kwani wamewanyanyua hata wale wenye hali ngumu ya kiuchumi.

“Tunamshukuru Saitoti kwa kutushirikisha nawapongeza wanachama wangu kwa kushiriki jambo hili kwa uwazi na kufuata utaratibu, wachimbaji wengine waige mfano wa Saitoti ili kunyanyua uchumi wa jamii,” amesema.

Mdau mwingine Boaz Ambonya amesema kampuni ya GEM & Rock ya Saitoti imefanya jambo jema kuendesha mnada huo kwani imeongeza wigo mpana wa uchumi wa mji mdogo wa Mirerani.

“Utaratibu wa kuendesha mnada umekaa vizuri kwani wanunuzi mnapewa namba kabla ya kuingia na unachukua madini yaliyopo kwenye alama utakachopata ndiyo riziki yako,” amesema.

Mwakilishi wa ofisa madini mkazi Mirerani (RMO) Seleman Ismail amesema mnada huo una faida mbili kwa serikali ikiwemo kuongeza mapato na wafanyabiasha kukata leseni.

“Mnada huu umekuwa na faida kwa wananchi na serikali kwani wafanyabiashara wameongeza vipato vyao na serikali imeongeza mapato na watu wengi wamekata leseni,” amesema.

Amesema wachimbaji wengine wanapaswa kufanya minada kama hiyo ili maono ya Waziri wa Madini, Antony Mavunde ya 2030 madini ni utajiri na maisha idhihirike kwa vitendo.

Related Posts