Wafanyabiashara Kagera, Morogoro nao wagoma, Songwe wakimbilia Zambia

MGOMO wa wafanyabiashara kutoka katika mikoa mbalimbali nchini imendelea kushika kasi baada ya mikoa ya Morogoro na Kagera kuungana na wengine wa mikoa nane kutofungua maduka yao.

Aidha, kwa upande wa Songwe wafanyabiashara na wananchi wa mji wa kibiashara wa Tunduma nao wamehamia upande wa pili wa nchi jirani ya Zambia ili kupata huduma. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Baadhi ya maduka halmashauri ya mji Tunduma yakiwa yamefungwa.

Akizungumza na MwanaHALISI leo Alhamisi, Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara bidhaa za Viwanda na Kilimo (TCCIA) wilayani Momba, Peter Mwamboneke amesema wanahitaji kodi rafiki sio kandamizi hasa ikizingatiwa mitaji yao inatokana na mikopo kutoka kwenye taasisi na benki mbalimbali.

“Asilimia 75 ya wafanyabiashara wenye maduka upande wa Nakonde nchini Zambia ni watanzania ambao wamekimbilia huko kufuata nafuu ya kodi na tozo” amesema Mwamboneke.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa wao ni wazalendo hawakutaka kukimbilia upande wa Zambia licha ya kuwa kunahuduma zote lakini wanaiomba serikali iangalie kwa jicho la tatu utatuzi wa changamoto za wafanyabiashara.

Related Posts