Biashara Tunduma zarejea maduka yafunguliwa

Wafanyabiashara wa mkoa wa Songwe katika masoko yaliyopo Tunduma wilayani Momba wameungana na wenzao wa mikoa mingine ikiwemo Kariakoo kufungua maduka baada ya serikari kuahidi kufanyia kazi changamoto zao.  Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea).

Hatua hiyo imekuja ikiwa zimepita siku tatu za mgomo wa wafanyabiashara hao kuanzia tarehe 24 hadi 27n  Juni mwaka huu, uliotikisa mikoa 10 ikiwamo Songwe.

MwanaHALISI Online imefika  na kuona shughulu zikiendeka huku maduka yakiwa yamefunguliwa na biashara zikiwa zinaendelea katika masoko yote.

Akizungumza leo tarehe 28 Juni mwaka, Mwenyekiti wa Chemba ya wafanyabiashara viwanda na kilimo wilayani Momba, Peter Mwamboneke amesema wameamua kufungua maduka baada ya serikali kuahidi kuyafanyia kazi na kupeleka kujadili changamoto hizo bungeni.

Amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilipa kodi na tozo kandamizi huku maofisa biashara na maofisa wa TRA wakishindwa kutoa elimu ya mlipa kodi kwa wafanyabiashara na kusababisha migongano.

Amesema hata halmashauri imekuwa ikitoza ushuru wa huduma bila kizingatia kipato cha mfanyabiashara huku kila kona wakiweka vizuizi vya kutoza kwa bidhaa za mkulima.

Amesema katika vizuizi hivyo kumekuwa na tozo ya Sh1000 kwa kila gunia 1 la mazao kinyume na agizo la serikali la bidhaa chini ya tani 1 kutotizwa ushuru.

“Serikali ilitangaza mazao ya mkulima tani 1 kushuka chini isilipiwe ushuru leo hii imekuwa ni chanzo muhimu cha halmashauri kuwanyonya wakulima, tunataka hili nalo lishughurikiwe,” amesema .

Mmoja wa wafanyabiashara wa mazao kutoka soko la Tunduma, Anneth Kayange amesema ndizi za kuiva, nyanya na maparachichi yameharibika na wameyatupa dampo kufuatia mgomo huo.

Amesema kwa sasa wanawaza namna ya kurejesha fedha kwani wanatumia fedha za mikopo kuendeshea biashara zao hivyo inawapa wakati mgumu kulipa.

Related Posts