CHUO CHA FURAHIKA WAONGEZA MUDA WA UDAHILI KWA WANAFUNZI WAPYA

CHUO cha Furahika Education College kilicho chini ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi -VETA kimeongeza siku za dirisha la usajili kwaajili ya kudahili wanafunzi wapya mpaka Julai 5, 2024.

Hayo ameyasema Mkuu wa chuo cha Furahika Education College Dkt. David Msuya wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 28, 2024. Amewakaribisha wanafunzi wa kutoka mikoa yote ya Tanzania kujisajili kusoma katika chuo hicho.

“Bado tunapokea wanafunzi wa mikoa yote ya Tanzania…. Tembelea website yetu ya www.furahika.or.tz au tembelea chuo kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam.” Ameeleza

Amesema katika chuo hicho kwa sasa wametengeneza maabara yakisayansi hivyo wanafunzi waliosoma masomo ya sayansi wasisite kuomba nafasi katika chuo hicho.

Maabara hii itawasaidia vijana wote wanaoomba kwaajili ya masomo ya sayansi na maabara hii inatarajiwa kuzinduliwa Julai 25, 2024, kwahiyo tunataka vijana wote wanosoma masomo ya Sayansi basi watakuja kubadilishana uzoefu nasi vitu mbalimbali kwaajili ya kujifunza katika chuo cha Ufundi cha Furahika kilichopo Buguruni Malapa katika Chuo Kikuu cha St. John.” Amesema Dkt. Msuya

Amesema kuwa amewaomba wazazi na walezi kuwapeleka watoto wa kike na wakiume nyumbani kwani Chuo cha Furahika kinamafunzo yote yanayotolewa na VETA.

Licha ya Hayo Dkt. Msuya ameomba jamii kuachana na ukatili wakijamii ili kila mmoja aishi maisha mazuri ya Amani na kufurahia kuwa Mtanzania.

Akitolea mfano wa Mtoto mwenye Ualbino aliyeuwawa hivi karibuni… Ninakemea vikali Vitendo vya Ukatili katika jamiii.. ninaiomba Serikali kufanya uchunguzi wa kina bila kulifanyia kazi, Vitendo hivi viko katika ngazi ya Mitaa, vijiji na kata sasa panapoonekana na vitendo vya namna hii maaana vinachafua taswira ya nchi yetu pale tunapokaribia uchaguzi wa Serikali za Mtaa au Uchaguzi Mkuu. Amesema Dkt. Msuya

Pia ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum iendelee kutoa elimu mara kwa mara bila kuangalia mjini au vijijini ili watu waelimike kuhusiana na ukatili unaoendelea katika jamii na kutoa taarifa ili wanaofanya hivyo waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Mimi kama balozi wa watoto naungana na Serikali kupinga Ukatili hapa nchini, wanaofanya ukatili, watu wanaofanya ukatili wa kuwauwa Maalbino. Niwaombe watanzania na mashirika yote hapa nchini kukemea Vikali ikiwa na kuwafichua wanafanya vitendo hivyo.

Pia Dkt. Msuya amewaomba watanzania kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mtaa na Uchaguzi mkuu kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura ili wakati unapofika kila mmoja aweze kumchagua kiongozi anayemtaka kwaajili ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Related Posts