REKODI mpya imewekwa kwenye mchezo wa mpira wa kikapu duniani, na hii imetokea kwenye Ligi ya NBA, baada ya jana Ijumaa, Los Angeles Lakers kumtambulisha kikosini mtoto wa nyota wa timu hiyo, LeBron James aitwaye, Bronny James kama mchezaji mpya wa timu hiyo msimu ujao.
Bronny alizua gumzo baada ya kuchaguliwa kutoka katika drafti namba mbili la wachezaji akiwa chaguo la 55 na anatarajiwa kucheza kwenye ligi ndefu pamoja na baba yake kwenye timu hiyo.
Kutokana na hilo, ni wazi sasa LeBron ataendelea kucheza kwenye timu hiyo baada ya siku za nyuma kudai ana ndoto ya siku moja acheze timu moja na mwanaye kabla hajastaafu na sasa ataongeza mkataba wa miaka mitatu zaidi ya kuichezea timu hiyo.
Bronny, mtoto wa Lebron kwa sasa ana umri wa miaka 19 wakati baba’ke anakwenda kucheza NBA msimu wa 22, hivyo inakwenda kuwa rekodi ya muda wote kwa ligi hiyo mchezaji kucheza na mwanaye timu moja.
RAUNDI YA PILI YA BRONNY
Wakati Bronny akichaguliwa namba 55, waliomtangulia mwanzoni kuanzia namba 31 ni Raptors kwa Jonathan Mogbo, Jazz kwa Kyle Filipowski, Bucks kwa Tyler Smith, Trail Blazers kwa Tyler Kolek aliyepelekwa Knicks, Spurs kwa Johnny Furphy akapelekwa Pacers, Pacers kwa Juan Nunez aliyepelekwa Spurs, Timberwolves kwa Bobi Klintman wakampeleka Pistons.
Knicks kwa Ajay Mitchell akapelekwa Thunder, Grizzlies kwa Jaylen Wells, Trail Blazers kwa Oso Ighodaro wakampeleka Suns kupitia Knicks, 76ers kwa Adem Bona, Hornets kwa KJ Simpson, Heat kwa Nikola Djurisic na kumpeleka Hawks, Rockets kwa Pelle Larsson na kumpeleka Heat, Kings kwa Jamal Shead na Rockets.
Clippers kwa Cam Christie, Magic kwa Antonio Reeves na kupelekwa Pelicans, Spurs kwa Harrison Ingram, Indiana Pacers kwa Tristen Newton, Pacers kwa Enrique Freeman, Knicks kwa Melvin Ajinca na kupelekwa Mavericks, Warriors kwa Quinten Post na anapelekwa Thunder, Blazers na kuishia Warriors, Pistons kwa Cam Spencer na kupelekwa Grizzlies, Celtics kwa Anton Watson, Suns kwa Kevin McCullar Jr na kupelekwa Knicks, Grizzlies kwa Ulrich Chomche anayeingia Raptors, Mavericks kwa Ariel Hukporti kupelekwa Knicks.