Mbowe: CCM wanajua uchaguzi huru, haki hawatoboi

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejiahakikishia ushindi katika chaguzi zijazo huku kikibainisha kuwa uchaguzi huru Chama cha Mapinduzi (CCM) hawatatoboa.

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa Juni 28, 2024 na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Freeman Mbowe, wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Dareda mjini Babati.

Chama hicho kinaendelea na mikikutano ya hadhara katika Kanda ya Kaskazini ikiwa ni sehemu ya Operesheni ya +255 Katiba Mpya pamoja na uimarishaji wa chama kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Akizungumza na wananchi hao Mbowe, amewataka kujipanga upya kwa kuwa wanazo mbinu za ushindi ili kukifundisha chama hicho tawala adabu kwa kuwa kimeshaishiwa pumzi.

 “Hebu kajipangeni upya mnajua uchaguzi wa vijiji na vitongoji mwaka huu, kata nzima ya Dareda na jirani tukawafundishe CCM adabu wanajua wao wameshaishiwa pumzi hawana uwezo wa kiushinda bila wizi, sisi tutashinda kwa mapemzi ya Mungu kwa muwa yupo upande wa wapenda haki,”amesema Mbowe.

Aidha Mbowe amewataka kutokata tamaa kwa kuwa mambo mazuri yanakuja akibainisha chama hicho kikuu cha upinzani kinakwenda kushindana na CCM, akieleza kuwa mwakani ndio mwisho wake.

Amesema CCM wanajua uchaguzi huru na wahaki hawawezi kutoboa, huku akilitahadharisha Jeshi la Polisi kutoegemea upande wowote wakati wa uchaguzi.

Awali, akizungumzia malalamiko ya wananchi Mbowe aliwata kurejesha Serikali ya kijiji, madiwani na wabunge wa Chadema ili kuweza kurekebisha kero hizo ambazo ni maudhi kwa miaka 63 baada ya uhuru.

  “Nimeambiwa kuna michango ya ujenzi wa shule kila Kaya Sh 54,000 na kuna vyumba vya madarasa havijakamilika hadi sasa, kuna matundu ya vyoo hayajakamilika tuliambiwa elimu ni bure, Serikali haina haja ya kudanganya kama haina waseme ukweli,”amesema Mbowe na kuongeza.

Kero nyingine aliyokutana nayo ni pamoja na kodi za majengo na michango ya miundombinu, ambapo kila wanaponunua umeme hukatwa bila kujali aina ya nyumba.

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini Godbless Lema amesema, ukiona sekemu yoyote duniani hakuna maendeleo kuna utawala usiofikiria.

Kwa kuwa tunawatu wasiowaza wala kufikiria eneo lililozungukwa na milima na misitu halipaswi kuwa na shida ya maji, wakati ukienda meneo mengine yaliyozungukwa na jangwa wana bustani katikati ya mji.

 “Tunakuaje na umaskini na shida ya huduma za jamii, mahali ambapo kuna utajiri wa kutosha unapokuwa angani ukiiangalia Manyara roho inaumaa ardhi yenye rutuba kama hii kila kitu kinaota, maeneo kama haya kwenye mataifa mengine kupata ardhi ni kazi ngumu sana,”amesema Lema.

Lema ambaye amewahi kuwambunge wa Arusha Mjini amesema, kamma yeye angekuwa sehemu ya Serikali jambo ambalo angelifanya ni kutengeneza benki ya wakulima ambayo ingetoa mikopo kwa wakulima wadogo.

Ametolea mfano eneo la Manyara na kusema endapo wananchi wangepata mikopo hiyo, wangeondokana na umaskini ndani ya kipindi cha miaka mitano.

 “Haya mambo yanawezekana yanahitaji watu makini na chama makini, sera yetu ya uchaguzi mwaka 2015/2020 mambo yote haya tumeyaeleza vizuri kabisa,”amesema Lema.

Kuhusu uchaguzi Lema amewataka wananchi kushirikiana na viongozi, kujiandikisha na kuwa na wito wa kushiriki siasa, kwa kuwa matatizo hubadilishwa na vyama vyenye sera nzuri.

Related Posts