NEMC YAHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA KISASA UCHENJUAJI WA DHAHABU

MKAKATI wa Kitaifa wa kupambana na matumizi ya zebaki umewasaidia maelfu ya wachimbaji wa dhahabu nchini kutambua matumizi salama ya zebaki na wengine kuachana nayo na kuamua kutumia teknolojia ya kisasa.

Ameyasema hayo leo Juni 28, 2024 Jijini Dar es Salaam Mratibu wa Mradi wa Kudibiti Zebaki wa NEMC, Dkt. Betrina Igulu, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya mkakati wa kitaifa kupunguza matumizi ya zebaki.

Amesema wachimbaji wengi wadogo wamekuwa wakipendelea zaidi matumizi ya zebaki kwenye kuchenjua dhahabu kutokana na urahisi wake wa kutumia na inapatikana kwa gharama nafuu zaidi.

Aidha amesema wamekuwa wakishirikiana na wadau mbalimbali kutoa elimu kuhusu madhara ya matumizi ya zebaki ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kuwafikia maelfu ya wachimbaji dhahabu mikoa mbalimbali nchini.

 “Tunasisitiza matumizi salama ya zebaki, kupunguza matumizi yake na ikiwezekana wachimbaji wadogo wa dhahabu waachane kabisa na njia hii watumie njia za teknolojia ya kisasa ili kupunguza madhara yanayopatikana kwa binadamu,” amesema

Amesema zebaki imekuwa ikipunguza uwezo wa kinga mwili hivyo kuwa katika hatari ya kupata magonjwa kama saratani na magonjwa mengine ambayo yamekuwa yakisababisha ulemavu wa kudumu.

Pamoja na hayo amesema wamekuwa wakiwafundisha wachimbaji wadogo matumizi sahihi ya zebaki na namna ya kuwa na teknolojia mbadala ya zebaki na kuwawezesha wachimbaji kuzitumia.

“Ukitumia zebaki kuchenjua dhahabu unaweza kupata asilimia 30 tu ya dhahabu wakati ukitumia teknolojia zingine za kisasa unaweza kupata hadi asilimia 90, wachimbaji wadogo wanapenda zebaki kwasababu ya urahisi wa upatikanaji wake lakini tunaendelea kuwaelimisha kuhusu madhara,” ameeleza

Dkt. Igulu amesema kuwa NEMC imefanikiwa kuziwezesha maabara nne kubwa nchini kupata teknolojia ya kisasa ya kuchenjua dhahabu ambayo watawawezesha wachimbaji wadogo kuipata ili waachane na maatumizi ya zebaki.

Amesema wamekuwa wakiwafundisha wachimbaji wadogo matumizi sahihi ya zebaki na namna ya kuwa na teknolojia mbadala ya zebaki na kuwawezesha wachimbaji kuzitumia.

“Ukitumia zebaki kuchenjua dhahabu unaweza kupata asilimia 30 tu ya dhahabu wakati ukitumia teknolojia zingine za kisasa unaweza kupata hadi asilimia 90, wachimbaji wadogo wanapenda zebaki kwasababu ya urahisi wa upatikanaji wake lakini tunaendelea kuwaelimisha kuhusu madhara,” amesema Dkt. Igulu.

Hata hivyo amesema teknolojia ya za kisasa zimekuwa zinatumiwa na wachimbaji wakubwa kutokana na gharama zake kuwashinda wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tafiti za Mazingira (NEMC), Dkt. Menan Jangu, amesema lengo la baraza ni kuhakikisha wachimbaji wanakuwa salama wakati wote wanapokuwa kwenye uchimbaji wa madini.

Amesema sekta ya madini inachangia fedha nyingi kwenye pato la taifa lakini upatikanaji wake umekuwa na athari kubwa kwenye mazingira kuanzia uchimbaji na uchakataji wake hasa wanapotumia kemikali ya zebaki.

“Lengo letu ni hizi shughuli zifanyike kwa namna ambayo haiathiri mazingira hapa nchini inakadiriwa kuwa kuna wachimbaji wadogo milioni moja na nusu sasa wakifanya akzi zao kwenye mazingira hatarishi watanzania wengi wataathirika,” amesema Dkt. Jangu.
Mratibu wa Mradi wa Kudibiti Zebaki wa NEMC, Dkt. Betrina Igulu, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya mkakati wa kitaifa kupunguza matumizi ya zebaki leo Juni 28, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mradi wa Kudibiti Zebaki wa NEMC, Dkt. Betrina Igulu, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya mkakati wa kitaifa kupunguza matumizi ya zebaki leo Juni 28, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mradi wa Kudibiti Zebaki wa NEMC, Dkt. Betrina Igulu, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya mkakati wa kitaifa kupunguza matumizi ya zebaki leo Juni 28, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Tafiti za Mazingira (NEMC), Dkt. Menan Jangu, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya mkakati wa kitaifa kupunguza matumizi ya zebaki leo Juni 28, 2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Related Posts