NHIF YAINGIA MAKUBALIANO NA ZHSF 

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Bw.Bernard Konga (kulia) na  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF),Yaasin Juma,wakisaini (kuhsoto) wakibadilishana  Mkataba wa mashirikiano ya utoaji huduma za Afya kati ya Taasisi hizo mbili ,hafla iliyofanyika leo Juni 28,2024 jijini Dodoma.

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Bw. Bernard Konga,akizungumza na waandishi wa habari  wakati akitoa taarifa ya kuingia Mkataba wa mashirikiano ya utoaji huduma za Afya na Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF),hafla iliyofanyika leo Juni 28,2024 jijini Dodoma.

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Bw. Bernard Konga,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari  wakati akitoa taarifa ya kuingia Mkataba wa mashirikiano ya utoaji huduma za Afya na Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF),hafla iliyofanyika leo Juni 28,2024 jijini Dodoma.

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF),Yaasin Juma, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuingia  Mkataba wa mashirikiano ya utoaji huduma za Afya na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) hafla iliyofanyika leo Juni 28,2024 jijini Dodoma.

 

BAADHI ya washiriki wakifatilia hotuba mbalimbali   wakati  Mkataba wa kusaini wa mashirikiano  utoaji huduma za Afya kati ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF),hafla iliyofanyika leo Juni 28,2024 jijini Dodoma.

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Bw. Bernard Konga (kulia) na  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF),Yaasin Juma (kushoto),wakisaini  Mkataba wa mashirikiano ya utoaji huduma za Afya kati ya Taasisi hizo mbili ,hafla iliyofanyika leo Juni 28,2024 jijini Dodoma.

WANASHERIA wakisaini makubaliano hayo.

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Bw.Bernard Konga (kulia) na  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF),Yaasin Juma,wakisaini (kuhsoto) wakibadilishana  Mkataba wa mashirikiano ya utoaji huduma za Afya kati ya Taasisi hizo mbili ,hafla iliyofanyika leo Juni 28,2024 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna -DODOMA

MFUKO  wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF), zimeingia Mkataba wa mashirikiano ya utoaji huduma za matibabu kwa wanachama wa ZHSF kupata huduma za afya wakiwa Tanzania Bara kuanzia Julai Mosi Mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kuingia mkataba huo jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bw. Bernard Konga, amesema hatua hiyo ni katika kuhakikisha ZHSF inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar Na. 1/2023.

Amesema kuwa hatua hiyo ni tekelezaji wa maamuzi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za matibabu wanapozihitaji bila kikwazo.

“Na kwa kutambua uzoefu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika uendeshaji wa mfumo wa bima ya afya nchini, Julai Mosi, 2024 ZHSF itaanza rasmi majukumu yake kwa kuhudumia wanachama na wategemezi wake kupitia vituo vya kutolea huduma vilivyosajiliwa na NHIF Tanzania Bara”amesema Konga

Aidha Konga,amesema  ili kufanikisha huduma kwa wanachama hao, NHIF na ZHSF zimesaini mkataba wa makubaliano wa mashirikiano katika utoaji wa huduma kwa wanachama wake.

“Hatua hii inatokana na uzoefu, wigo mpana wa vituo vya kutolea huduma vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima”amefafanua Konga

Amesema NHIF, imekamilisha hatua mbalimbali za maandalizi na utayari wa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa mashirikiano ili kuhakikisha wanachama hao wanapata huduma bila ya changamoto yoyote.

Hata hivyo ameeleza kuwa  hatua ilizokamilisha NHIF ni pamoja na kutoa taarifa kwa watoa huduma wote kuhusu suala hilo na kuwa tayari kuwahudumia wanachama.

 “Ofisi zote za NHIF zilizoko katika mikoa ziko tayari na zimejipanga kutoa huduma na kutoa msaada utakapohitajika.”amesisitiza

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa ZHSF, Yaasin Juma, amesema  kwa mujibu wa kifungu cha 27 cha Sheria Nam.1 ya 2023, Mfuko umepewa uwezo wa kuwafikishia wanachama wake huduma za afya nje ya Zanzibar.

Bw.Juma amesema kwa kuanzia ZHSF imeanza kuwafikia wanachama wake walioko Tanzania Bara.

“Tukio la leo linaakisi utekelezaji wa masharti ya Sheria hiyo. Hivyo basi, mafanikio haya ya kufikia makubaliano na wenzetu wa NHIF ni ya kujivunia kwani yatawawezesha wanachama wetu kupata huduma za afya wakiwa Tanzania Bara kwa kutumia kadi za ZHSF”amesema

Aidha amesema  wanategemea mashirika yao kama ZIC, PBZ ambayo yanafanyakazi Tanzania Bara na wategemezi ambao wachangiaji wao wapo Zanzibar watafaidika na huduma hizo.

Related Posts