Huu utakuwa mkutano wa tatu, ambao unaongozwa na Umoja wa Mataifa huko Doha, lakini ni mara ya kwanza kuhudhuriwa na Taliban, ambayo haitambuliwi kimataifa tangu kunyakua mamlaka Agosti 2021, ikiwa ni baada ya vikosi vinavyoongozwa na Marekani kuondoka katika ardhi ya Afghanistan baada ya miaka 20 ya vita.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukijaribu kutafuta mbinu ya pamoja yenye kujumuisha mataifa mengi katika kukabiliana na Taliban, ambao wamechukua mwelekeo mkali katika kubinya haki za wanawake tangu kurejea kwao madarakani.
Nikimnukuu Tirana Hassan ambae ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la kimataifa lenye kutetea haki za watu, Human Rights Watch anasema “Kuwatenga wanawake kuna hatari ya kuhalalisha unyanyasaji wa Taliban na kusababisha madhara yasiyoweza kurekebishwa katika kuaminiwa kwa wa Umoja wa Mataifa kwa juhudi zake za utetezi wa haki za wanawake na umuhimu wa ushiriki wa wanawake.”Vizuizi dhidi ya wanawake vyazidi kuitenga Afghanistan na jumuiya ya Kimataifa
Umoja wa Mataifa umesema mkuu wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarlo, Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Afghanistan Roza Otunbayeva na wajumbe kutoka mataifa mbalimbali wanatarajiwa kukutana kwa nyakati tofauti na mashirika ya kiraia ya Afghanistan, ikiwa ni baada ya kukutana na Taliban.
Jumapili iliyopita Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric amesema mikutano ya Doha wa Juni 30 ni “sehemu ya mchakato na sio jambo lamara moja” kadhalika wanawake na jumuiya za kiraia zitaendelea kuwa sehemu yake.”
Dujarric aliongeza kwa kusema. “Haki za binadamu na haki za wanawake na wasichana itaangaziwa katika mijadala yote.”
Tangu Taliban warudi madarakani, wasichana wengi wamekuwa kuzuiliwa kujiunga na masomo ya shule za upili na wanawake kujiunga na vyuo vikuu. Wataliban pia wamewazuia wafanyakazi wengi wa kike wa Afghanistan kufanya kazi katika masharika ya misaada, saluni zilizofungwa, wanawake wamezuiliwa kujitokeza katika maeneo ya wazi kama bustani, kuzuiwa kwa safari za wanawake pasipo´uwepo wa mwanaume kando.Afghanistan yawazuia wasichana kutoendelea na shule
Taliban wanasema wanaheshimu haki wanawake kulingana na tafsiri zao sheria ya Kiislamu.
Otunbayeva anasema mkutano wa Doha utazingatia sekta ya biashara na elimu na dawa za kulevya na masuala yenye kuhusishwa na wanawaeke. Anasema mkutano huo ntarajiwa kutoa matarajio mengi muhimu ambayo matokeo yake hayawezi kuidhihirisha wazi kwa mkutano mmoja.Taliban yakataa kushiriki mkutano kuhusu Afghanistan
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alikutana kwa mara ya kwanza wajumbe wa Afghanistan kutoka nchi mbalimbali mwezi Mei mwaka jana kwa lengo la kufanyia kazi mbinu ya umoja wa mataifa katika kukabiliana na mamlaka ya Taliban. Taliban hawakualikwa.
Itakumbukwa kuwa ule mkutano wa pili, mamlaka ya Taliban iligoma kuhudhuria baada ya Umoja wa Mataifa kuzuia ombi lake la kutaka kutambuliwa rasmi kama mwakilishi pekee katika mkutano huo wa Februari. Mkutano hup kadhalika ulifanyika mjini Doha, Qatar.