SERIKALI imewaagiza waganga wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia kwa karibu upatikanaji wa dawa kwa wananchi hasa wazee,wamekuwa wakisosa dawa muhimu wanapokwenda kutibiwa hospitalini.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda,ameagiza leo wakati akifunga mkutano wa mwaka wa MSD uliohusisha wateja na wadau,waganga wa mikoa na wilaya,wafamasia na waatalamu wa maabara kutoka mikoa ya Mwanza,Geita,Shinyanga,Simiyu na Mara.
Amesema yapo malalamiko ya wazee wanapokwenda hospitali kutibiwa wakiandikiwa dawa muhimu hawazipati,wanaambiwa wakanunue kwa sababu wajanja wachache wanazichepusha wakitumia takwimu za makaratasi kuonesha zimewafikia walengwa,hivyo waganga wakuu wa mikoa na wilaya wakasimamie upatikanaji wa dawa kuhakikisha zinawafikia wananchi.
Mtanda amesema kazi waganga hao ina tija,ni ya kizalendo na moja ya majukumu yao ni kusimamia dawa ziwafikie wananchi lakini wengine huko mitaani wana maduka ya dawa, wanazichepusha na kuzipeleka huko na kuwataka wafuatilie kwa kuwa mambo hayo yanafanyika chapu chapu (haraka haraka).
“Tunaosimamia sera za afya na matibabu ya wazee,watumishi wakiwaona wazee kwenye madirisha ya dawa wanafikiri wakipewa ni hasara,hivyo hawapewi wanaambiwa wakanunue,wakati zinaletwa na serikali na kumbe wenye misamaha unajaza fomu za dawa hizo una request fedha serikalini,”amesema.
Aidha Mtanda amegusia baadhi ya vituo kuomba dawa nyingi kuliko idadi ya watu zinaisababishia serikali hasara baada ya miezi mitatu muda wake wa matumizi kwisha zinapoteza ubora na hivyo waganga wa mikoa waziondoe kwa utaratibu na kuzipeleka kwenye idadi ya watu wengi.
Mkuu huyo wa mkoa ameahidi serikali itaendelea kushirikiana kutatua changamoto za MSD ukiwemo udhibiti wa uchepushaji wa dawa,hivyo madhumuni ya majadiliano ya mkutano huo yalenge kuboresha uhusiano na ushirikiano ili kuleta tija na akufanye utendaji uwe bora.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari la Dawa (MSD),Mavere Tukai ameeleza kuwa,miaka miwili iliyopita walikuwa wakidaiwa sh.bilioni 159 na wateja,wamelibadilisha deni hilo kuwa bidhaa ambapo inawadai wateja sh.bilioni 69 hadi mwaka huu wa fedha ulioisha.
“Tunalenga watu wapate dawa ambapo tumefikia zaidi ya asilimia 80,tunatakiwa kuboresha zaidi huduma lakini mvua zimeharibu miundombinu ya kufikisha dawa kwa wateja,gari inachukua siku mbili hadi nne kuzifikisha kituo,hivyo mamlaka zinazohusika na barabara zitimize wajibu wake,”amesema Tukai.
Naye mwakilishi wa OR-TAMISEMI, Zuberi Abdallah ameeleza katika kuongeza ufanisi vifaa tiba vinavyosambazwa na washitiri vipitie MSD wavifahamu ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa re-argent vinapoharibika pia, kiwango cha fedha kiongezwe ili kufikisha mzigo (bidhaa za afya) vituoni.
Awali Mkurugenzi wa Uendeshaji wa MSD,Victor Sungusia amesema mkutano huo unalenga kuboresha mnyororo ghafi wa huduma za afya na kuhakikisha zinawafikia wananchi kwa ubora ili kufikia adhima ya serikali.
“Tunaowapa huduma wanapozikosa uzuri wote wa huduma ulizowahudumia zinaonekana bure hakuna kilichofanyika,hivyo juhudi zinazochukuliwa na serikali zinatupa matumaini kuwa chini ya miaka tutafanya vizuri sababu ya uwekezaji uliofanyika katika sekta ya afya,”amesema.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari la Dawa (MSD), Mavere Tukai akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, leo wakati wa mkutano mkuu wa mwaka uliohusisha wateja,wadau, watumishi wa umma wa sekta ya afya na watumishi wa MSD..
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Shirati KMT,Dr.Bwire Chirangi akichangia mada katika mkutano wa mwaka wa MSD na wateja,wadau,watumishi wa sekta ya afya na watumishi wa bohari hilo la dawa,leo jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Said Mtanda akifunga mkutano wa mwaka wa MSD, wadau na wateja (hawapo pichani) jijini humu leo.