TETESI ZA USAJILI BONGO: Yusuph Mhilu ajiandaa kurejea Kagera Sugar

KLABU ya Kagera Sugar imeanza mazungumzo ya kumrejesha aliyekuwa mshambuliaji nyota wa kikosi hicho, Yusufu Mhilu kwa ajili ya kukipigania kuanzia msimu ujao.

Mchezaji huyo aliyeibuliwa na Yanga kisha kuzichezea Ndanda na Simba, aliwahi kuichezea Kagera Sugar, kabla ya msimu uliomalizika hivi karibuni kukipiga Geita Gold iliyoshuka daraja akiifungia mabao matatu katika Ligi Kuu Bara na sasa mabosi  wa klabu hiyo ya zamani wa Kagera wanataka kumrudisha kuendelea kuwasha moto.

Akiwa na Kagera msimu wa 2019-2020 Mhilu aliibuka mfungaji bora namba mbili wa Ligi Kuu akitupia mabao 13, nyuma ya Meddie Kagere aliyekuwa Simba aliyemaliza na 22, kisha msimu uliofuata wa 2020-2021 alifunga mabao tisa kabla ya Simba kumnasa.

Related Posts