Tisa wafikishwa mahakamani mauaji ya Asimwe

Bukoba. Watuhumiwa tisa mauaji ya mtoto mwenye ualbino Asimwe Novath (2) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba leo Juni 28, 2024.

Mei 30, 2024, mtoto Asimwe aliporwa kutoka kwa mama yake na watu wasiojulikana kisha wakatokomea naye. Juni 17, 2024, ikiwa ni siku 18 tangu alipochukuliwa, Asimwe alikutwa mabaki ya mwili huku baadhi ya viungo vikiwa vimenyofolkewa.

Maofisa wa Polisi wakichukua mabaki ya mwili wa mtoto mwenye Ualbino, Asimwe Novath (2) yaliyopatikana siku 19 tangu mtoto huyo apokwe katika mikono ya mama yake mzazi na watu wasiyojulikana. Picha na Ananias Khalula.

Juni 19,2024  Jeshi la Polisi lilitoa taarifa ya kuwashikilia watu tisa kwa tuhuma hizo akiwemo Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bugandika wilayani Misenyi Mkoa wa Kagera, pamoja na baba mazazi wa mtoto huyo.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Related Posts