Uvivu na kutofanya mazoezi ni chanzo cha maradhi – DW – 28.06.2024

Takriban watu bilioni 1.8 wamo katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya saratani, kiharusi, kisukari na kupoteza kumbukumbu kutokana nakutofanya mazoezi ya kutosha.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema katika ripoti yake kwamba kutofanya mazoezi ya viungo kumeongezeka duniani kwa asilimia tano kuanzia mwaka 2010 hadi 2022, lakini karibu asilimia 31ya watu wazima bado hawafanyi mazoezi ya mwili.

Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida la The Lancet Global Health, ulionyesha kuwa asilimia 34 ya wanawake na 29 ya wanaume wanabweteka tu. Ikiwa mwelekeo wa sasa utaendelea, asilimia 35 ya watu duiani watabweteka hadi ifikapo 2030.

Daktari wa Ujerumani akimpima mgonjwa wa kisukari, Nairobi Kenya
Daktari wa Ujerumani akimpima mgonjwa wa kisukari, Nairobi KenyaPicha: Miro May/picture alliance

“Kutofanya mazoezi ya mwili ni tishio la kimya kimya kwa afya ya duniani na huchangia kwa kiasi kikubwa mzigo wa magonjwa sugu,” Hayo amesema mkurugenzi wa kitengo cha kuendeleza afya Ruediger Krech, wa shirika la afya duniani, WHO.

Mkurugenzi huyo amesema hatari ya magonjwa yasiyoambukiza inaweza kupunguzwa “kwa kufanya mazeozi ya mwili na kuleta faraja.

Shirika la afya duniani WHO linapendekeza mazoezi ya mwili hata wakati wa mapumziko na linapendekeza dakika 150 za mazoezi au wastani wa dakia 75 kila wiki. Soma: Njia za kupunguza uzito

Ingawa shughuli za wastani za kila siku ni pamoja na kutembea haraka haraka au kufanya  shughuli nzito za usafi kama vile kusafisha madirisha au kupiga deki, shughuli za nguvu ni pamoja na kupanda mlima, kukimbia na kushika koleo.

WHO: Unene unachangia magonjwa mengi

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Mkurugenzi mkuu wa shirika la WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema utafiti mpya umebainisha fursa iliyopotea katika kupunguza maradhi ya saratani, magonjwa ya moyo, na kuimarisha afya ya akili kwa njia ya mazoezi ya mwili.

Amesema pana haja ya kujizatiti upya katika kuongeza mazoezi ya mwili kwa njia ya kuimarisha sera na kuongeza fedha ili kuepuka mkondo huo wa hatari. Utafiti: Saratani za chini ya miaka 50 zaongezeka

Shirika la afya WHO linapendekeza wastani wa dakika 75 za mazoezi kila wiki kwa watu wazima, kama kukimbia au kushindana katika michezo. Mkurugenzi wa kitengo cha  kuendeleza afya kwenye shirka la WHO amesema bila ya kuusgughulisha mwili, mtu atakuwamo katika hatari ya kukumbwa na maradhi ya moyo, saratani na kisukari.

Mambo kadhaa yanayosababisha watu kutofanya mazeozi ni pamoja na baadhi ya watu kutumia muda mwingi kwenye kompyuta, kutazama televisheni kwa muda mrefu badala ya kufanya mazoezi. Watu wanatakiwa wajishughulishe badala ya kukaa vitini tu.

WHO yazindua mikakati ya kupambana na Saratani ya kizaziMakadirio ya sasa ya kimataifa yanaonyesha kuwa thuluthi moja ya watu wazima na asilimia 81 ya vijana hawafanyi shughuli za kutosha za kimwili. Zaidi ya hayo, kadiri nchi zinavyoendelea kiuchumi, viwango vya kutofanya kazi za nguvu huongezeka na vinaweza kuwa vya juu hadi  kufikia asilimia 70 kutokana na mabadiliko ya mifumo ya usafiri, kuongezeka kwa matumizi ya teknolojia kwa ajili ya kazi na burudani na pia kutokana na maadili ya kitamaduni na kuongezeka kwa tabia ya kubweteka. 

 

Related Posts