WADAU WATAKIWA KUWEKEZA NGUVU YA PAMOJA MAPAMBANO DHIDI YA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA ZANZIBAR

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Bi Harusi Sadi Suleiman, akimkabidhi cheti cha shukrani Rukia Salim Afisa Kinga masuala ya UKIMWI kutoka Amref Tanzania wakati wa kongamano la kuadhimisha siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya lilofanyika kisiwani Pemba, Zanzibar 27-06-2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Bi, Harusi Sadi Suleiman, akifungua kongamano la siku moja la kupiga vita matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya Zanzibar, lililoandaliwa na Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa dawa za kulevya, kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, lililofanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba 27-06-2024

 

***

 

Amref Tanzania kupitia ufadhili wa Kituo cha Serikali ya Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) Tanzania) imeungana na Serikali kupitia Wizara ya Afya Zanzibar, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya Zanzibar (ZDCEA), Wadau na Wataalam mbalimbali katika Kongamano la kujadili mipango na mikakati ya kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya Zanzibar Tanzania.

 

Kongamano hilo limefanyika  Juni 27,2024 katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba ambapo maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya Zanzibar yamefanyika chini ya kauli mbiu; “Ushahidi Upo Wazi Tuwekeze Katika Kukinga”.

 

Kupitia ufadhili wa Serikali ya Marekani CDC Tanzania, Amref Tanzania inashirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar, ZDCEA na wadau wengine katika kutoa huduma za waraibu ambapo huduma za Medication-Assisted Treatment (MAT) hutolewa kwa waraibu wa dawa za kulevya katika hospitali ya Kidongo Chekundu Zanzibar.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar Bi Harusi Sadi Suleiman akiwa Mgeni rasmi amewataka wadau, kuendelea kuunganisha nguvu za pamoja kwenye mapambano dhidi ya tatizo hilo ili kutokomeza kabisa Matumizi ya Dawa za Kulevya Zanzibar.

Washiriki wa Kongamano la siku moja la kupiga Vita matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya Zaznibar, wakifuatilia kwa makini kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba 27-06-2024.

Washiriki wa Kongamano la siku moja la kupiga Vita matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya Zaznibar, wakifuatilia kwa makini kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba 27-06-2024.

Washiriki wa Kongamano la siku moja la kupiga Vita matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya Zaznibar, wakifuatilia kwa makini kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba 27-06-2024.

Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi, Bi Harusi Sadi Suleiman, katika kongamano la siku moja la kupiga vita matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya Zanzibar, lililoandaliwa na Tume ya Kitaifa ya kuratibu na Udhibiti wa dawa za kulevya, kutoka Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais, lililofanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba 27-06-2024

Related Posts