DC kilosa Shaka Hamdu Shaka ataka wananchi kutunza miradi ya maendeleo

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa shaka hamdu shaka amewataka wananchi wa kata za Ulaya na Zombo kutunza Miundombinu ya miradi Mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

DC shaka ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Miradi inayotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la WORLD VISION TANZANIA tarafa ya ulaya (ULAYA AP) halfa ambayo imefanyika Kijiji Cha Madudumizi kata ya Zombo

DC shaka amesema serikali na wadau Mbalimbali zimekua zikitekeleza ujenzi wa Miradi Ili kusaidia huduma wananchi hivyo ni jukumu la kila mtu kuilinda Ili isiharibike ambapo amewapongeza shirika ilo Kwa kujenga Miradi ya afya,elimu na maji katika tarafa hiyo .

Kwa upande wake Meneja WORLD VISION TANZANIA kanda ya Kati na nyanda za juu Kusini Pudensiana Rwezaula amesema Miradi hiyo imeanza kutekelezwa mwaka 2015 na kukabidhiwa rasmi Juni 27 mwaka huu na kuhusisha mradi wa ujenzi wa zahanati , vifaa tiba na madarasa 4 ,jengo la utawala na kisima cha maji Kijiji cha madudumizi , katika Kijiji Cha zombo umetekelezewa mradi wa maji

Pudensiana ametaja miradi mwingine ni katika Kijiji Cha Ulaya Mbuyuni uboreshaji mradi wa maji na miradi yote ikiwa na Thamani zaidi ya Shilingi milioni mia sita huku Mratibu wa mradi wa maendeleo Ulaya Kilosa Shirika la World Vision Elisei Chilala amesema kukamilika kwa miradi hiyo ni ushirikiaano mzuri wa serikali na Wananchi.

Kwa upande wake meneja wa RUWASA mkoa Morogoro Mhandisi Sospiter Lutonja amesema Hali ya upatikanaji wa maji katika wilaya hiyo ni asilimia 60 ambapo tayari miradi mbalimbali inatekelezwa yenye Thamani zaidi ya bilioni 8 lengo kufikia asilimia 85 hadi ifikapo mwaka 2025.

Nao ,Amina Jongolo na Zaina Hassan* wakazi wa Kijiji cha madudumizi kata ya Zombo wanasema kupatikana kwa zahanati hiyo imekua mkombozi kwao kwani awali walikua wakijifungulia njiani kutokana na zahanati kuwa mbali pamoja kunywa maji pamoja na mifugo kwa kukosa mambomba lakini kwa sasa wanashukuru shirika la *WORLD VISION* Kwa upatikanaji wa huduma hizo karibu.

 

 

Related Posts