TANZANIA WASAINI MKATABA KULISHA ZAMBIA

 

Mkurugenzi wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Andrew Komba na Mratibu wa Taifa la Zambia, Rouben Mtolo Phiri wakibadlishana mikataba mara baada ya kusaini mikataba kwaajili ya kuuziana mahindi meupe tani 650,000. Mikataba hiyo imesainiwa jijini Dar es Salam leo Juni 29, 2024.
Mkurugenzi wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Andrew Komba na Mratibu wa Taifa la Zambia, Rouben Mtolo Phiri wakisaini mikataba kwaajili ya kuuziana mahindi meupe tani 650,000. Mikataba hiyo imesainiwa leo Juni 29,2024.
Waziri wa Fedha Mwigulu Mchemba akizungumza wakati wa kusaini Mkataba kati ya Tanzania na Zambia kwaajili ya kuuza mahindi Me upe tani 650,000. Mkatab huo umesainiwa leo Juni 29, 2024 jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Kilimo Husein Bashe akizungumza wakati wa kusaini Mkataba kati ya Tanzania na Zambia kwaajili ya kuuza mahindi Me upe tani 650,000. Mkatab huo umesainiwa leo Juni 29, 2024 jijini Dar es Salaam.

SERIKALI kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), imesaini mkataba na Serikali ya Zambia kwa ajili ya kuuza tani laki sita na nusu za mahindi nchini humo kwa kipindi cha miezi nane
Kusainiwa kwa mkataba kunafuatia serikali ya Zambia kutangaza kukumbwa na baa la njaa lililosababishwa na ukame.
Wakisaini hati hizo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameihakikishia Zambia kuwa tani laki sita na nusu watazipata kwa wakati bila vikwazo vyovyote.
Bashe ameongeza kuwa kuanzia Julai 10 mwaka huu NFRA itafungua vituo kwa ajili ya ununuzi wa mahindi kwa bei nzuri kutoka kwa wakulima na kwamba lengo la serikali kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025 ni kununua wastani wa tani milioni 1.1
Akishuhudia kusainiwa kwa hati hizo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hatua ya Tanzania kuuza mahindi nchini Zambia itasaidia nchi kupata fedha za kigeni ambapo nchi inatarajia kupata zaidi ya dola za Marekani milioni 250 kutokana na mauzo ya mahindi hayo
Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo wa Zambia, Reuben Mtolo Phiri amesema mikoa nane ya Zambia ambayo huzalisha chakula kwa wingi imepata changamoto ya ukame, hatua ambayo imesababisha upungufu mkubwa wa chakula nchini humo.
Mahindi kutoka Songwe, Mbeya, Sumbawa ga na Songea ndio yanayotarajiwa kusambazwa nchini Zambia na NFRA.

Related Posts