WATAALAMU WA USAFIRISHAJI MSD WAJENGEWA UWEZO

Wataalamu wa Usafirishaji wa Bohari ya Dawa (MSD) wameendelea kujengewa uwezo kupitia mafunzo mbalimbali yanayohusu Kada yao ya usafirishaji yanayoandaliwa na taasisi.

Wataalamu hao wanapatiwa mafunzo katika maeneo mbalimbali yakiwemo Afya ya Akili, udereva wa kujihami, alama za barabarani, ukaguzi wa magari, sheria za usalama barabarani, upakiaji wa mizigo na namna bora ya kuendesha magari makubwa yanayovuta tella (truck and trailers) ili kuongeza tija katika kazi zao na taasisi kwa ujumla.

Mafunzo hayo ya siku tatu yanafanyika mkoani Dodoma yanahusisha nadharia na yanatolewa na wataalamu kutoka taasisi mbalimbali.

Akifungua Mafunzo hayo Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu – Wizara ya Afya Ndg. Issa Ng’imba ameipongeza MSD kwa kuratibu mafunzo hayo, kwani yatakua na tija kwa wataalamu wa usafirishaji.

“Nawaomba mtakayojifunza hapa yaende kuisaidia MSD kuongeza tija katika utendaji wake kwani MSD kwa kiasi kikubwa inawategemea nyinyi katika utekelezaji wa jukumu la usambazaji wa bidhaa za afya alisema Ndg. Ng’imba


Ng’imba ameongeza kuwa kazi ya udereva ni kazi ngumu sana inahitaji ustahimilivu wa hali ya juu wakati mwingine hata kujihami dhidi ya watumia barabara wasio waadilifu.

Tunatamani kuendelea kuona madereva wa MSD wanakuwa mfano wa kuigwa aliongeza Ndg. Ng’imba

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Mavere Tukai katika wasilisho lake alitoa mfano wa Ndg. Jarufu Ngolo Dereva wa MSD Kanda ya Iringa ambaye amefanyakazi kwa muda mrefu wa takribani miaka 28 na ametembea kilometa nyingi na hivyo kutengeneza thamani katika utendaji wake.

Utendaji mzuri wa MSD unaongezeka kutoka na utendaji wenu uliotukuka lakini kwa mapungufu machache yanayojitokeza basi tuhakikishe tunajirekebisha ili kuhakikisha tunaendelea kutunza jina la MSD katika nyanja ya usafirishaji Alisema Mavere.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa MSD Mboyi Wishega amesema MSD inatambua umuhimu wa kada ya usafirishaji ndio maana kila mwaka MSD inaandaa mafunzo kwa wataalamu hao.



Related Posts