Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Pwani akijadiliana jambo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega katika Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Jengo la Shughuli za Kiuchumi za Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani iliyofanyika jana tarehe 29 Juni katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam.Katika tukio hilo, watu mbalimbali wakiwemo wa chama na serikali walihudhuria.