Kura mbili zamhamishia Mch. Msigwa CCM

Aliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini na mjume wa zamani wa kamati Kuu ya Chadema, Mchungaji Peter msigwa leo tarehe 30 Juni 2024 amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hiko na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Msigwa amepokewa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), kilichokutana jijini Dar Es Salaam leo tarehe 30 Juni 2024 chini ya Rais Samia.

Hayo yanajiri ikiwa imetimia mwezi mmoja tangu Msigwa  abwagwe na Mbunge zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu katika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa.

Mchungaji Peter Msigwa

Katika uchaguzi wa kanda hiyo uliofanyika tarehe 29 Mei mwaka huu kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makambako, ambao ulikuwa na mchuano mkali, Sugu aliibuka kidedea baada ya kupata kura 54 sawa na asilimia 51 dhidi ya Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliyepata kura 52 (asilimia 49).

Hata hivyo, tarehe 3 Juni mwaka huu Msigwa alitangaza kukata rufaa kwenye Kamati Kuu ya Chama Chadema kupinga ushindi huo wa Sugu.

Kutokana na malalamiko ya Msigwa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Amosi Makalla alimshauri Msigwa ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, ahamie CCM kutokana na malalamiko ya kutotendewa haki kwenye Uchaguzi wa Uenyekiti wa CHADEMA Nyasa uliompa ushindi Sugu.

Makalla alisema “Msigwa amesema ‘najitokeza hadharani kuwaeleza Watanzania na CHADEMA sisi muda wote tumehoji Tume ya Uchaguzi kumbe sisi ni waongo hata sisi wenyewe hatufuati taratibu za uchaguzi Mimi nimeonewa nimeibiwa kura’ sasa na Mimi namuambia Msigwa pole sana Mchungaji njoo CCM ambako kuna demokrasia tele, kuna uwazi”

“Umeonewa pole sana Mchungaji Msigwa hicho Chama hakikufai tena njoo CCM, amesema tunawadanganya tu Watu kuhusu Katiba, Tume ya Uchaguzi kumbe Chama chetu hakifuati hata sheria za uchaguzi za Chama chake” alisema Makala.

Related Posts

en English sw Swahili