Manji afariki dunia, Yanga wamlilia

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yusuf Manji amefarikia dunia leo Jumapili jijini Florida nchini Marekani baada ya kuugua kwa muda mfupi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Uongozi wa Young Africans Sports Club umethibitisha kifo cha Manji ambaye alikuwa mfadhili wa timu hiyo kuanzia 2012 hadi 2017 Mei alipojiuzulu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Klabu ya Yanga imesema imepokea hiyo kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Manji aliyewahi kuwa Mdhamini na Mwenyekiti wa Klabu.


“Kifo cha Marehemu Manji kimetokea leo, Juni 30. 2024, nchini Marekani alipokuwa akipatiwa matibabu “ imesema taarifa hiyo.

Rais wa Young Africans Sports Club, Eng Hersi Said amesema enzi za uhai wake, Yusuf Manji alikuwa kiongozi mahiri aliyejituma na kujitoa kwa ajili ya kuijenga KIabu ya Yanga.

“Hi ni pigo kubwa kwetu Young Africans Sports Club na familia ya michezo kwa ujumla. Tutamkumbuka Yusuf Manji kwa mapanzi yake makubwa aliyokuwa nayo kwa Klabu yetu na namna alivyokuwa akijitoa kwa hali na mali katika kuiendeleza sekta ya michezo Tanzania,” amesema Rais Eng, Hersi Said.

Manji alihudumu katika nafasi mbalimbali za kiuongozi ndani ya Klabu ya Yanga  kama Mdhamini na Mwenyekiti ambapo hadi umauti unamkuta alikuwa Mwanachama wa Young Africans Sports club.

“Uongozi wa Young Africans Sports Club, unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wanamichezo wote nchini kwa msiba mzito wa mpendwa wetu.

“Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe pho ya Marehemu mahala pema Peponi, Amina. Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea,” amesema.

Related Posts

en English sw Swahili