MABOSI wa Yanga wanadaiwa wapo kwenye mazungumzo ya kumuongezea mkataba mpya kiungo nyota wa timu hiyo, Pacome Zouzoua.
Kiungo mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast alijiunga na timu hiyo Julai 19 mwaka jana akitokea Asec Mimosas ya nchini kwao na amebakisha mkataba wa mwaka mmoja, hivyo kuzivutia klabu mbalimbali za ndani na nje ya nchi jambo. Tayari mabosi wa Yanga wameanza mazungumzo ili kumaliza utata.
Katika msimu wa kwanza wa kuichezea Yanga, Pacome ameifungia mabao saba ya Ligi Kuu na kuasisti mara tatu, huku katika Ligi ya Mabingwa Afrika ndioye kinara wa timu akifunga mabao matatu na asisti moja.